Uvinza Fm

Waliopokea chanjo ya uviko 19 afya zao ni salama

11/08/2021, 7:29 pm

Na,Timotheo Leornadi

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Ruchugi kata ya Uvinza wilayani Uvinza Mkoani Kigoma ambao tayari wamepokea chanjo ya UVIKO -19 wamesema ni salama kwa afya, nakwamba wale ambao bado wanamitazamo hasi wakachajwe  kulinda maisha yao

Hayo wameyasema kwa nyakati tofauti ndani ya kijiji hicho wakati Redio Uvinza fm ilipotaka kujua maendeleo ya wananchi ambao tayari wamepokea chanjo na wale ambao hawajapokea chanjo hiyo

Sauti za wananchi

Kwa upande wake mganga Mkuu wa Wilaya ya Uvinza BI: ZAITUNI HAMZA amesema hadi sasa hawajapokea malalamiko yoyote kuhusu chanjo hiyo huku akisisitiza wananchi kuendelea kuchanja

Sauti ya Mganga mkuu uvinza

Hata hivyo Daktari Hamza ameendelea kusema kuwa takwimu kwa maeneo ambayo wamefika kutoa chanjo ndani ya wilaya ya uvinza  zimeongezeka tangu walipoanza zoezi hilo

Sauti ya Mganga mkuu uvinza

Aidha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania MH. SAMIA SULUH HASAN hivi karibuni alizindua chanjo ya corona kwa kuchanjwa yeye kwanza ilikuwathibitishia watanzania kuwa hakuna madhara kwa watakaoitumia.