Uvinza Fm

Waziri wa TAMISEMI aziagiza halmashauri kuongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato

07/07/2021, 4:49 pm

Na,Glory Paschal

Waziri wa nchi ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa Tamisemi Ummy Mwalimu ameziagiza halmashauri za Mkoa wa Kigoma kuongeza ukusanyaji wa Mapato pamoja na kuhakikisha mapato yanayokusanywa yanatumika kutatua changamoto za wananchi

Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu akizungumza na sekritarieti Kigoma

Akizungumza na Sekritarieti ya mkoa wa Kigoma Ummy Mwalimu amesema hali ya ukusanyaji wa mapato kwa halmashauri mkoani hapa bado iko chini Ukilinganisha na malengo ya serikali kwa mwaka wa fedha kama ambavyo takwimu za makusanyo kuanzia mwezi januari mpaka machi zinavyoonesha

Amesema licha ya ukusanyaji wa mapato kuwa chini lakini matumizi ya fedha hizo katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo hairidhishi na kusababisha kuendelea kwa changamoto kwa wananchi

Sauti ya Waziri Ummy Mwalimu

Akitoa taarifa ya Mkoa wa Kigoma Mkuu wa mkoa huu Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye amesema katika changamoto zinazokumba mkoa huo kada ya afya inaongoza kwa kuwa na upungufu wa watumishi wanaofikia asilimia 76.9.

Sauti ya mkuu wa mkoa Kigoma

Akizungumzia changamoto hiyo Waziri Ummy Mwalimu amesema katika ajira mpya mkoa wa Kigoma utapata watumishi wa afya karibu 140 sanjari na ujenzi wa vituo vya afya

Sauti ya waziri Ummy Mwalimu

Aidha katika sekta ya Elimu Ummy Mwalimu amesema serikali itajenga shule mpya za sekondari 11 katika kata mkoani hapa pamoja na umaliziaji wa maboma ya madarasa yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi.