Uvinza Fm

Wananchi Waomba Muongozo Chanjo ya Corona

05/07/2021, 5:43 pm

Na,Glory Paschal

Wananchi wilayani kasulu mkoani kigoma wameiomba  serikali kuharakisha  kutoa  muongozo wa chanjo ya virusi vya corona ili waweze kupata elimu zaidi kuhusu chanjo hiyo ya virusi vya corona ambayo wamekuwa wakiisikia kutoka nchi jirani

Mganga Mkuu wilaya ya kasulu

Wamesema hayo Wakati Wakizungumza na Redio  Uvinza fm, ilipotembelea Mjini humo  ambapo wamesema kumekuwa na propaganda nyingi kutoka kwa baadhi ya watu juu ya chanjo ya virusi vya corona hali inayowapa hofu katika kupata chanjo hiyo

sauti za wananchi

Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya kasulu Dr. Peter Njanga amesema kuwa hadi sasa miongozo juu ya chanjo itakayotumika hapa nchini haijatoka hivyo kuwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari zilizotolewa mpaka hapo wizara ya afya  itapotoa miongozo kuhusu chanjo ya virusi vya covid19

Kwa upande  wake katibu mkuu wizara ya afya maendeleo ya jamii Prof. Abel Makubi amesema kuwa  tayari kuna muongozo  maalumu ambao unaandaliwa na serikali  katika kusimamia  Chanjo  na utakapokuwa tayari utawekwa wazi kwa kila mwananchi

Sauti ya katibu wizara ya afya