Uvinza Fm

Wakazi wa Matendo watembea umbali mrefu kufuata maji

04/06/2021, 7:51 pm

Na,Glory Paschal

Wananchi wa Kijiji cha Pamila Kata ya Matendo Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, Wameiomba  Serikali  kuwasaidia kupeleka huduma ya maji kwani wanalazimika kutembea umbali mrefu kutafuta maji na kushindwa kufanya shughuli za maendeleo

Wakizungumza  na  Radio  Uvinza Fm, Wananchi hao wamesema kwa muda mrefu wamekuwa wakitumia maji ya visima jambo ambalo linasababisha  kuendelea  kusumbuliwa  na  magonjwa ya mlipuko

Sauti za wananchi wa pamila

Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Pamila Adam Senga na Rulai Bakari mwanyekiti wa Kitongoji hicho wamesema tatizo la maji katika kijiji hicho limedumu kwa takribani zaidi ya miaka 15 na wananchi hulazimika kutumia maji yaliyotuwama

Sauti ya mwenyekiti

Naye diwani wa Kata ya Matendo  Issa  Ramadhani amesema tayari kata hiyo imetengewa fedha  ambayo itatumika kufikisha huduma ya maji katika kata hiyo

Sauti ya diwani

Kwa Upande wake Meneja wa Mamlaka ya maji Safi na Usafi wa Mazingira vijijini Ruwasa Halmashauri ya Wilaya Kigoma Respisius Mwombeki  amekiri Kijiji cha Pamila kukaa kwa muda mrefu bila huduma ya maji

Sauti ya meneja wa maji safi kigoma