Uvinza Fm

Serikali kutenga fedha kwa ajili ya kutengeneza barabara

28/05/2021, 7:15 pm

Na,Rosemary Bundala

Serikali imesema itaendelea kutenga fedha katikaWizara ya ujenzi  ili kuzifanyia matengenezo barabara korofi  kwa kadri upatikanaji wa fedha utakavyokuwa unaendelea  kuimarika

Naibu waziri wa nchi ofisi ya Rais (TAMISEMI)

Hayo yamejili leo bungeni jijini Dodoma wakati naibu waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mikoa na serikali za mitaa(TAMISEMI) Mh David Silinde alipokuwa akijibu swali la mbunge wa kigoma kusini mh Nashon William Bidyanguze lililohoji je serikali ina mpango gani wa kujenga barabara tatu za lukoma lubalisi, kaliya, lubanda na kaliasibwe zinazounganisha mkoa wa kigoma  kupitia wilaya ya uvinza

 

Sauti ya naibu waziri wa nchi ofisi ya Rais(TAMISEMI)

Aidha katika hatua nyingine mh Silinde amesema katika mwaka wa fedha 2019/2020 barabara za lukoma , lubalisi,kalia lubanda na kalia sibwesa zilitambuliwa na wakala wa barabara za vijijini na mijini TARURA  na kuwekwa kwenye mfumo unaotambuliwa na TARURA na barabara hizo zitaingizwa kwenye mpango wa matengenezo ya barabara kupitia fedha za matengenezo ya barabara zinazotolewa na TARURA katika kila halmashauri

Sauti ya naibu waziri ofisi ya Rais (TAMISEMI)

 

Katika hatua nyingine naibu waziri amesema kuwa serikali kwa kushirikiana na wananchi  pamoja na shirika la maendeleo la ubeligiji la kuendeleza kilimo kigoma linaendelea na ujenzi wa madaraja kumi kwa kutumia tekinolojia ya mawe  kwa gharama ya shilingi milioni 190 ambapo madaraja matatu yamekamilika likiwemo daraja la mto luega katika barabara ya kalia lubanda lililojengwa kwa shilingi milioni thelathini na saba katika mwaka wa fedha 2019/2020

Sauti ya naibu waziri ofisi ya Rais (TAMISEMI)