Uvinza Fm

Wananchi waiomba Serikali kudhibiti maeneo hatarishi

27/05/2021, 4:55 pm

Na,Glory Paschal

Wananchi Mkoani Kigoma wameitaka Serikali kudhibiti maeneo hatarishi ya mito na mabwawa machafu yanayochochea ongezeko la magonjwa ya kichocho na minyoo hasa kwa watoto

maji machafu yanayochochea magonjwa

Wamesema maeneo mengi yamejaa maji Machafu hivyo ni muhimu elimu ikatolewa kwa kuwashirikisha wananchi  na serikali  za  mitaa  na vijiji ili kuokoa maisha ya watu ambayo yapo hatarini kutokana na hali hiyo

Sauti za wananchi

Mratibu wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele Mkoani Kigoma Emmanuel Bihongora amesema katika kukabiliana na magonjwa ya minyoo na kichocho watatoa dawa kwa watoto kuanzia umri wa miaka mitano kuhakikisha wanadhibiti magonjwa hayo

Sauti ya mratibu wa magonjwa yasiyopewa kipaumbele

Kwa upande wake  mwakilishi wa mkuu wa mkoa wa Kigoma ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Buhigwe Kanali Michael Ngayalina ameitaka jamii kutumia fursa hiyo kuhakikisha watoto wote wanapata dawa ili kudhibiti magonjwa yasiyopewa kipaumbele

Sauti ya mkuu wilaya ya Buhigwe