Uvinza Fm

Serikali kuboresha mifumo ya upatikanaji wa pembejeo

26/05/2021, 7:28 pm

Na,Rosemary Bundala

Serikali imesema  imenza kuboresha mifumo ya upatikanaji wa pembejeo kwa maana ya mbolea mbegu na viwatilifu ,kuratibu mahitaji ya pembejeo kutoka katika mikoa na kuweka mazingira wezeshi kwa ajili ya makampuni kupeleka na kuuza

Naibu waziri wa kilimo Hussein Bashe

Hayo yamejiri leo bungeni Jijini Dodoma wakati naibu waziri wa kilimo Hussein Bashe  akijibu swali la mbunge wa viti maalumu Bi. Stela Simon Fiayo lililohoji je ni lini serikali italeta pembejeo za kilimo zenye bei nafuu ili wananchi waweze kuzimudu

Sauti ya Naibu waziri wa kilimo

Aidha naibu Bashe amesema kuwa mikakati mingine ni kuanzisha mifumo ya uhalamiaji wa sekta hasa ikiwemo uanzishwaji wa mfuko wa pembejeo(credit quarantee scheme) pia kufuta na kupunguza baadhi ya tozo na ada kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita serikalli imepitia na kufuta tozo kumi na mbili katika mbegu na tozo nne za mbolea ili kupunguza bei na gharama za pembejeo hizo

 Hata hivyo  Naibu waziri  Bashe Amesema Serikali  inaendelea kutekeleza Mikakati ya upatikanaji wa pembejeo kwa kuvutia wawekezaji wa makampuni binafsi hasa katika eneo la mbegu na mikataba maalumu kwa ajili ya kupunguza gharama

Sauti ya naibu waziri wa kilimo

Bunge limeendelea leo Jijini Dodoma ambapo wabunge wanaendelea kujadili bajeti ya Wizara ya Kilimo kwa Mwaka wa fedha 2021/22 ambayo ni kiasi cha Shilingi bilioni 294.1.