Uvinza Fm

Makubaliano ya Mkataba wa Mdomo yanyoshewa kidole

07/05/2021, 1:28 pm

Na, Timotheo Leonardi

Mkurugenzi wa kituo cha msaada wa usaidizi wa kisheria Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma Joseph Kanyaboya amewaomba waajiri wa Wafanyakazi wamajumbani, kuhakikisha kuwa wanazingatia taratibu za makubaliano kwanjia ya Mkataba wamaandishi, badala ya makubaliano ya Mdomo akiyataja kuwa yanaweza kumnyima haki Mfanyakazi

Pichani ni Mfanyakazi wa Nyumbani

Hayo ameyasema wakati akiongea na Radio Uvinzafm ilipotaka kujua nikwanamnagani wafanyakazi wamajumbani wanavyoweza kupata haki zao wakati wengiwao hufanyakazi pabila kuwa na Mikataba

Sauti ya Msaidizi wa kisheria

Kwa upande wake Aloka Mashaka Mama Mjasiriamali anayeishi na Mfanyakazi amekiri kuwa yeye hana Mkataba wowote wamaandishi kiasi kwamba huweka makubaliano yeye na wazazi wa Mtoto jambo ambalo anasema nikweli sirahisi Mfanyakazi kupata haki zake

Sauti ya mwajiri Aloka Mashaka

Naye Neema Salvatory ambaye anafanyakazi za nyumbani licha ya kufanyakazi bilakuwa na Mkataba amesema pesa anazozipata zimesaidia kuendeleza ujenzi Nyumbani huku akishauri  wale wanaoishi na Wafanyakzi kuendelea kuwajari

Sauti ya Mfanyakazi Neema Salvatory

Hata hivyo Kufanyakazi kwa makubaliano ya maandishi ya Mkataba ni moja ya mambo yanayo himizwa katika kupunguza migogoro baina ya wafanyakazi pamoja na waajiri kwani kukiwa na maandishi nirahisi mtu kupata haki zake