Uvinza Fm

Sehemu yakufanyia Biashara yawaliza Wajasiriamali

05/05/2021, 3:49 pm

Na, Timotheo Leonardi

Baadhi ya Wajasiriamali wa Kijiji cha Uvinza kata ya Uvinza Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma, wamesema wanapata adhaa kubwa wakati wakifanya shughuli zao kutokana na kukosekana kwa eneo maalum la kuuzia bidhaa zao

Sehemu ya kuuzia Biashara

Hayo Wameyasema mbele ya kinasasauti cha Redio Uvinza fm mara baada ya kuwatembelea kujionea hali halisi ya Soko hilo, nakuiomba Serikali kuwatazama kwa jicho la tatu kutokana na eneo hilo kutokuwa rafiki kwa shughuli zakibiashara.

Sauti ya Wajasiriamali

Kwa upande wake Jonathan Manyaga ambaye ni Mwenykiti wa Wafanyabiashara amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo, nakuiomba serikali kusikia kilio cha Wajasiriamali hao, kwa kuimarisha suala la usafi pamoja na kuboresha miundombinu ya soko

Mwenyekiti wa Wafanya Biashara

Naye Diwani wa Kata ya Uvinza Aloka Mashaka amesema  tayari Shiling Milioni Arobaini zimeshaidhinishwa  kwa mwaka  wa Fedha 2020-2021 kwaajili ya kuwajengea eneo la kuuzia bidhaa zao kwa uhuru

Sauti ya Diwani

 Aidha kupatikana kwa soko kwaajili ya kufanyia Biashara kutasaidia Wafanyabiashara wengi kuvutiwa na hatimaye kujiongezea kipato maradufu.