Uvinza Fm

Jumuiya ya Dini yatoa pongezi kwa Rais Samia Suluhu

28/04/2021, 6:18 pm

Na,Glory Paschal

Jumuiya ya Dini Mbalimbali Mkoani kigoma imetoa Pongezi kwa Mh. Rais Samia Suluhu  kwa  kuwa  Rais wa Tanzania na kuvipa nafasi vyama vya siasa vya Upinzani kupata fursa ya kuonana nae na kuzungumzia mwenendo wa Siasa Nchini

Pichani ni wanajumuia kigoma

Jumuiya hiyo inahusisha dini ya Kiislamu na kikristo pamoja na madhehebu ya pande zote mbili lengo likiwa ni kuendelea kudumisha amani, umoja na Upendo katika kulijenga Taifa

Sauti ya ya Askofu wa PAGT

Kisha pongezi kwa Mh rais Samia Suluhu Hassan kwanza kwa hotuba yake aliyotoa bungeni iliyoonyesha dira ya Tanzania ambayo kila mwananchi anatamani kuifikia lakin kubwa Zaidi ni mustakabali wa siasa nchini kwa kutoa nafasi ya kukutana na viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani

Sauti ya Askofu wa kanisa la PAGT

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Kamishna wa Polisi Thobias Andengenye na Mkuu wa Wilaya Uvinza wakapongeza jitihada ambazo zimekuwa zikifanywa na viongizo wa dini na kuwaomba kuendeleza juhudi za pamoja kuhakikisha malengo ya serikali yanatimia.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa na mkuu wa Wilaya Uvinza