Uvinza Fm

Ushirikiano hafifu chanzo cha ukatili wakijinsia Mkoani Kigoma

22/04/2021, 5:24 pm

KIGOMA

Na, Glory Kusaga

Jumla ya Kesi  881 za vitendo  vya unyanyasaji wa kijinsia Mkoani Kigoma zimeripotiwa kwa kipindi cha kuanzia mwezi Oktoba Mwaka jana hadi Machi 2021 huku kesi  138 tu ndizo zimefika mahakamani huku changamoto ikitajwa kuwa ni ushirikiano hafifu wa jamii kutoa taarifa za vitendo hivyo

Mahakama kuu ya Kanda ya kigoma

Hayo yamebainishwa na Mratibu wa Dawati la Jinsia mkoa wa Kigoma Inspekta Doris William Sweke wakati wa kikao kilichowakutanisha wadau wa masuala ya ukatili Mkoani kigoma ambapo amesema kesi nyingi hazifanikiwi kutokana na jamii kuchelewa kutoa taarifa za watu wanaotekeleza ukatili huo

Sauti ya mratibu wa Dawati

Naye hakimu mkazi wa Mahakama ya Wilaya Kigoma Eva Mushi amesema kesi nyingi zimekuwa zikichelewa kutolewa hukumu kutokana na ucheleweshwaji wa ushahidi kutoka kwa mhanga wa matukio ya ukatili

Sauti ya hakimu mkazi

Kwa  upande wake Mgeni rasmi wa Mkutano huo  Moses Msuluzya ambaye amemwakilisha Katibu tawala wa Mkoa wa Kigoma amesema ni wajibu wa viongozi kuwa kitu kimoja kushughulikia kesi za ukatili

Sauti wa muakilishi wa RAS Kigoma

Nao baadhi ya wadau wa kupinga vitendo vya ukatili Mkoani Kigoma wamesema ukatili umekithiri kutokana ulevi uliopindukia kwa wazazi na walezi

Sauti ya wadau wa ukatili Kigoma