Uvinza Fm

Mafuriko yakumba Kaya 50

18/04/2021, 8:56 am

KIGOMA

Na; Glory Kusaga

Takribani kaya 50 zilizopo Kata ya Katubuka manispaa ya kigoma ujiji Mkoani Kigoma zimekumbwa na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani kigoma.Baadhi ya waathirika Wamesema changamoto ya maji kukaa katika makazi yao ni kubwa na kuiomba serikali kutuma wataalamu kuwasaidia kutatua changamoto hiyo.

Maji ya mvua yametuama katika makazi ya watu

Ni miezi miwili  sasa tangu eneo hilo kuanza kujaa maji ambapo kulingana na historia kumekuwa na bwawa ambalo kila mwaka wakati wa mvua maji hujaa lakini kwa mwaka huu hali imezidi kuwa mbaya zaidi kiasi cha kuhatarisha maisha ya wakazi wa eneo hilo.

Wananchi wakizungumzia kero hiyo

wataalamu kutoka manispaa ya Kigoma ujiji wamefika eneo hilo kujionea hali halisi na kuzungumza na waathirika , ikaibuka hoja ya kuwahamisha  kutoka eneo hilo baada ya kukosekana namna nyingine bora Zaidi ya kuwasaidia kuepukana na adha hiyo.

Sauti za wataalamu wa manispaa

Diwani wa kata ya katubuka Moshi Mayengo anaeleza kwasasa hatua iliyochukuliwa kuokoa wakazi waliopata mafuriko hayo ni kuwahamisha kwa majirani huku hatua za ziada zikiendelea kuchukuliwa.

Sauti ya diwani wa Katubuka