Uvinza Fm

Wananchi wa Nkungwe wilayani Kigoma washukuru serikali kwa kuondoa kero ya maji.

24/03/2021, 10:48 am

KIGOMA.

Wananchi wa Kata ya Nkungwe Halmashauri ya Wilaya Kigoma Mkoani Kigoma wamepongeza Serikali kuwasaidia kuwapelekea huduma ya maji kwani kwa muda mrefu wamekuwa wakitumia maji ya visima  hali iliyosababisha kuungua magonjwa ya mlipuko mara kwa mara.

wananchi wakichota maji katika moja ya gati la maji nkungwe

Wananchi hao wameeleza hayo wakati wa ufunguzi wa wiki ya Maji katika kata hiyo ambapo wamesema kwa muda mrefu wamekuwa wakitumia maji ambayo yalikuwa yanawasababishia kupata magonjwa ya kuhara.

Sauti za wananchi wa Nkungwe wakiishukuru serikali kwa kupata maji.

Naye Mhandisi wa Maji safi na Ufasi wa Maazingira Vijijini Ruwasa Resipisus Mwombeki amesema tatizo la ukosefu wa maji katika kata hiyo lilisababishwa na ukosefu wa mashine za kusukuma maji kuyafikisha kwa kila kijiji.

Sauti ya meneja wa Ruwasa akizungumzia mradi huu.

Amesema hata hivyo Serikali imeamua kubadilisha mfumo wa matumizi ya mashine za kusukuma maji na kuweka sola ambazo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kwani zina uwezo wa kusukuma  maji lita 450 kwa siku.Hata hivyo Mgeni Rasmi katika ufunguzi wa siku ya Maji Mkuu wa Wilaya Kigoma Samson Anga amewataka wananchi kuilinda na kuhifadhi miundombinu hiyo ya maji ili iweze kudumu na kutoa maji kwa wananchi muda wote.

Sauti ya dc kigoma akiwaasa wananchi kuutunza mradi huo.