Tumbatu FM

Kaskazini Unguja yashauriwa kupinga vitendo vya udhalilishaji

28 September 2021, 2:11 pm

Mkutano wa jumuiya ya kupambana na udhalilishaji kaskazini unguja.
Na Vuai Juma.

Uingijaji wa wageni kiholela ndani ya mkoa wa kaskazini Unguja ndio chanzo cha kuwepo Utelekezaji wa familia.

Na Vuai Juma.

Serekali ya mkoa wa kaskazini unguja imeshauriwa kuweka mikakati Madhubuti kwa wageni wanaoingia katika  maeneo ya mkoa huo ili kuondoa vitendo vya utelekezaji katika jamii.

Ushauri huo umetolewa katika ukumbi wa skuli ya mahonda na mwanyekiti wa mtandao wa kupinga vitendo vya udhalilishaji mkoa wa kaskazini unguja bi Hadia Ali Makame katika kikao cha  kujadili muenendo wa matukio hayo.

Hata hivyo alisema kuwa wamekuwa na kesi nyingi za kutelekeza hasa katika maeneo ya madago pamoja na sehem za  kitalii hivyo ni vyema kwa serekali kuweza kuandaa sheria ambazo zitasaidia  kusimamia  tamaduni za maeneo husika.

Aliongezea kwa kusema kuwa wageni wengi wanaokuja katika maeneo hayo huingia kwa lengo la kufanya biashara za kuanika madagaa na nyenginezo ambazo zinakubalika kisheria lakini mwishowake hujiingiza katika masuala ya kuuza mili yao jambo ambalo linapelekea kuzaliwa Watoto ambao wanakosa huduma na kuishia kutelekezwa.

Kwaupane wake mjumbe wa mtandao huo bi Asia Fadhil Makame alisema athari nyingi zinapatikana kwa Watoto waliokosa malezi ya pamoja kwani wengi wao huishia kuingia katika makundi maovu jambo ambalo  huhatarisha Maisha ikiwemo ulevi,ubakaji,maradhi ya usongo wa mawazo pamoja na kujiingiza katika vitendo vya ushoga.

Nae msaidizi wa sheria kutoka wilaya ya kaskazini “B” Bwana Omar Khamis amesema chanzo kikubwa kinacho pelekea kuongezeka kwa watu wanao telekeza familia zao ni ukosefu wa elimu ya ndoa ambayo inakosekana kwa wanandoa walio wengi.

Aidha ameishauri jamii kuweka utaratibu maalum wa kuwapatia vijana elimu hiyo  kabla ya kuowa kwani itashajihisha kuweza kuondoa vitendo hivyo na jamii kubaki salama..

Kikao hicho ni mwendelezo wa vikao vinavyofanywa na mtandao huo katika kuendeleza jitihada za kuhakikisha kuwa vitendo vya udhalilishaji vinapungua katika mkoa huo.

Na Vuai Juma