Triple A FM

MAWAZIRI WATATU KUSHIRIKI MAADHIMISHO ARUSHA.

8 November 2021, 12:50 pm

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. John Mongella

Na.Anthony Masai,Arusha

Mkuu wa Mkoa Arusha, John Mongella amewataka wananchi wa Jiji hilo kutumia wiki ya kupambana na magonjwa yasioambukiza kwa kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya upimaji afya pamoja na kupata ushauri wa kitaalamu.

Bwana Mongella amesema, maadhimisho hayo yanayofanyika nchi nzima, Kitaifa yanatarajiwa kuadhimishwa Arusha  katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, huku Waziri wa Afya Doroth Gwajima akitarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Aidha ameeleza kwamba maadhimisho hayo yanatarajiwa kufunguliwa Novemba 6 na Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo Innocent Bashungwa.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa ameongeza kuwa,Waziri Ummy Mwalimu pamoja na Waziri Joyce Ndalichako watahudhuria maadhimisho hayo yatakayoanza Novemba 6 hadi 13.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bwana John Mongella akizungumzia magonjwa yasiyoambukizwa

Pamoja na hayo, Bwana Mongella amesema shughuli zitakazofanyika ni upimaji wa afya, mazoezi, ushauri wa kuwa na mtindo mzuri wa maisha ikiwa ni pamoja na elimu ya vyakula.

mwisho.