Storm FM

Upatikanaji wa huduma za afya bado ni changamoto.

4 August 2021, 4:54 am

Na Mrisho Sadick:

Halmashauri ya mji wa Geita bado inakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma za afya kwa baadhi ya maeneo kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo upungufu wa watumishi pamoja na kushindwa kukamilika kwa majengo ya Zahanati.

Hayo yamebainishwa na Kaimu Mganga Mkuu wa halmashauri ya Mji wa Geita Dk Anath Mussa katika kikao cha robo ya nne cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo ambapo amesema licha ya uwepo wa changamoto hiyo wameendelea kupambana kuhakikisha wanazipunguza kwa kutumia CSR.

Baadhi ya Madiwani katika kikao hicho hawakuridhishwa na majibu ya kaimu mganga  Mkuu ambapo wameishauri halmashauri hiyo kutumia mapato ya ndani kutatua changamoto ya huduma za afya badala ya kusubiri fedha za CSR.

Kutokana na kukosekana kwa majibu ya moja kwa moja juu ya utatuzi wa changamoto ya huduma za afya kutoka idara ya afya,Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Geita Rashid Mhaya akatoa msimamo wa serikali.