Storm FM

Tunatambua mchango wa wawekezaji:

7 July 2021, 8:26 pm

Mgodi wa uchimbaji wa madini ya dhahabu wa Busolwa Mining uliyopo kata ya Nyarugusu wilayani Geita umeahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika Nyanja mbalimbali za kimaendeleo ikiwemo kutatua changamoto zinazowakabili wakazi wa kata hiyo.

Akizungumza mara baada ya kutembelewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita ,Meneja Mwajili wa Mgodi huo Bw Masumbuko Thobias amesema Mgodi huo ni sehemu ya jamii, na wamekuwa wakishiriki katika shughuli mbalimbali za maendeleo  ikiwemo Elimu , Afya na Miundombinu.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe, Rosemery Senyamule ameupongeza Mgodi wa Dhahabu wa Busolwa Mining kwa uwekezaji huo nakuwashauri watu wengine kuendelea kujitokeza  mkoani Geita kufanya uwekezaji.

ROSEMERY SENYAMULE – RC GEITA

Sambamba na hilo Mhe, Senyamule ameuhakikishia uongozi wa mgodi huo na migodi mingine kuwa, serikali iko nyuma yao kuhakikisha inatatua changamoto mbalimbali zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi.