Storm FM

Mkoa wa Chato wapendekezwa kuundwa na wilaya 5

26 May 2021, 2:17 pm

Kikao cha kamati ya ushauri cha mkoa wa Geita (RCC) kimekubaliana kwa pamoja kuwa mkoa mpya  wa Chato  utakaomegwa kutoka katika mkoa wa Geita na mikoa jirani za kagera na kigoma utaundwa na wilaya tano za Chato,Bukombe,Ngara,Bihalamulo na kakonko.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe, Rosemery Senyamule

Kikao hicho kilianza kwa wajumbe wa kikao kujadili namna ya mkoa huo utakavyoundwa na mapendekezo ya awali yalikuwa mkoa mpya wa chato uundwe na wilaya sita za Chato,Bukombe,Ngara,Bihalamulo, Busanda na kakonko.

Mvutano katika mgawanyo huo ulikuwa katika wilaya ya Chato na Geita ambapo chato ilikuwa ikipendekeza wilaya mpya ya Busanda ikaunde mkoa wa chato huku wilaya ya Geita ikitaka hifadhi ya taifa ya Rubondo iende wilaya ya Geita.

Baada ya makubaliano ya pamoja Mkuu wa mkoa wa Geita Mhe, Rosemery Senyamile akatangaza kuwa mkoa mpya wa Chato utaundwa na wilaya tano ambazo ni Chato,Bukombe,Ngara,Bihalamulo na Kakonko huku mkoa wa Geita ukibaki na wilaya za Geita,Mbogwe,Busanda na Nyangwale.