Storm FM

Wachimbaji Watakiwa Kuondoa Migogoro Kazini

21 May 2021, 5:52 pm

Na Joel Maduka:

Wachimbaji wadogo   ambao wamekuwa wakifanya shughuli zao kwenye  Mikoa  ya Kanda ya ziwa  wametakiwa  kuondoa tofauti  ambazo zimekuwa zikisababisha migogoro ya mara kwa mara  hali inayochangia  kushindwa kuungana ili  kuweza kukuza uzalishaji wao na kuufanya kuwa wenye tija kutokana na mchango  mkubwa ambao wamekuwa wakiutoa  kwenye sekta ya  uchumi wa taifa.

Hayo yamebainishwa   na Mkuu wa Wilaya ya Kahama Anamringi Macha wakati akifungua Mafunzo kwa waandishi wa habari kutoka  Mikoa ya Geita, Mwanza  na Shinyanga ambayo yameandaliwa na taasisi ya kuendeleza uchimbaji mdogo FADEV ambapo lengo lake ni kusaidia  kuandika habari  ambazo zitawasaidia wachimbaji wadogo kufata kanuni na sheria za uchimbaji salama.