Storm FM

Wagoma kulinda usiku kwa kuhofia kukamatwa

21 April 2021, 12:00 pm

Na Mrisho Sadick:

Mtaa wa Nyamakale uliyopo halmashauri ya mji wa Geita Mkoani Geita unakabiliwa na changamoto ya ulinzi shirikishi  kutokana na baadhi ya wakazi wa eneo hilo kushindwa kushiriki kwa madai ya kuogopa kupata matatizo.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Nyamakale Bw Enoi Tito

Wakizungumza na Storm FM baadhi ya wakazi wa Mtaa huo wamesema kuwa licha ya kutokuwepo kwa matukio makubwa katika mtaa huo wanaogopa kushiriki ulinzi shirikishi kutokana na tukio lililotokea mwaka 2004 la baadhi ya polisi jamii kukamatwa na kufungwa jela kwa madai ya mauaji.

Wananchi Nyamakale

Katika hatua nyingine wamesema ili wakazi wa eneo hilo waendelee kushiriki nivyema viongozi wa serikali ya mtaa wawe bega kwa bega na wananchi hususani pale wanapofikwa na changamoto wakiwa katika ulinzi.

Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa huo Bw Enoi Tito aliechaguliwa mwaka 2019 amewaondoa wasiwasi wakazi wa mtaa huo kwakusema kuwa ulinzi shirikishi katika eneo hilo nimuhimu na wasahau yaliyopita.