Storm FM

Watoa huduma ya chakula mitaani watakiwa kuvaa sare Geita

15 April 2021, 5:50 pm

Na Kale Chongela:

Watoa huduma ya chakula katika halmashauri ya mji wa Geita wametakiwa kuvaa mavazi maalum wakati wa biashara pamoja na kofia kwa ajili ya kuimarisha usafi  ili kuendelea kulinda afya za wateja wanaowahudumia.

Wito  huo umetolewa  na Afisa Afya wa kata ya Mtakuja Bw Edward Mwita ambapo amebainisha kuwa  ni vyema kuendelea kuzingatia  suala la mavazi kwa watoa huduma ya chakula  ili kuimarisha usafi  sambamba na kuepukana na magonjwa ya mlipuko.

Afisa Afya

Wakielezea baadhi ya watoa huduma kwenye migahawa wamesema  licha ya uwepo wa changamoto  ya kiuchumi wameahidi kuzingatia taratibu na kanuni ambazo zinatolewa na idara ya afya ili kuweza kuepukana na mvutano.

Aidha baadhi ya wananchi mjini Geita wamesema endapo suala la usafi wa mazingira likizingatiwa katika huduma za utoaji wa chakula itasaidia kuondokana  changamoto ya magonjwa ya mlipuko.