Storm FM

Tukuze Utalii wa ndani sisi wenyewe

15 April 2021, 6:23 pm

Na Mrisho Sadick:

Katika kukuza utalii wa ndani baadhi ya walimu wa shule za msingi na sekondari Mkoani Geita wameungana kwa pamoja  kuchangia ziara ya  mafunzo katika Hifadhi za Taifa  kwa lengo la kujijengea uwezo wa kitaaluma kuhusu rasilimali hizo.

Akizungumza na Storm Fm Mwakilishi wa   walimu wa Sekondari kwenye Chama cha walimu  Tanzania CWT wilaya ya Geita Mwalimu Gipson  Petro   amesema zaidi ya walimu 90 wamechangia kutembelea hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro.

Ametoa wito kwa walimu wa shule za msingi na sekondari pamoja na makundi mengine katika jamii ikiwemo madaktari kuchangamkia fursa hiyo kwani ziara hiyo inalenga kuwajengea uwezo wa kitaaluma kuhusu masuala ya uhifadhi.

Mwalimu Gipson Petro

Mwalimu  Grassian Ntaleka  wa Shule ya Msingi Igenge  na Mwalimu Faraja  Manyawa  wa Shule ya Msingi Bombambili mjini Geita wamesema ziara hiyo itawasaidia kuwajengea uwezo wa kufundisha masuala yanayohusu maliasili na utalii.