Storm FM

Wafugaji wakaidi kuchukuliwa hatua kali Geita

14 April 2021, 4:02 pm

Na Kale Chongela

Serikali ya mtaa wa Tambukareli kata ya kalangalala Halmashauri ya mji wa Geita  imeanza utekelezaji wa kuwachukulia hatua kali wafugaji ambao hawazingatia  taratibu na kanuni za ufugaji maeneo ya mjini.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Bw Mabula Ndoshi  akizungumza na Storm FM Ofisini kwake baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wakulima wanaodai kuharibiwa mazao yao na mifugo , amesema kumekuwepo na baadhi ya wafugaji ambao hawazingati taratibu na kanuni za ufugaji hali ambayo inasababisha malalamiko mengi baina ya wakulima na wafugaji nakwamba ofisi yake itaendelea kuchukua hatu kali ili kuodoa changamoto hiyo.

Mwenyekiti wa Mtaa

Miongoni mwa wakulima walioharibiwa mazao yao na mifugo nakufika katika ofisi ya serikali ya mtaa huo Bw Mwembeki Dickson  amesema mazao yake mahindi , marando ,mihogo na migomba yameharibiwa vibaya na mifugo aina ya Ngo’ombe na Mbuzi nakuuomba uongozi wa mtaa huo kuingilia kati kutatua mgogoro huo.

Aidha baadhi ya wafugaji katika mtaa huo wamekiri kuwepo kwa changamotyo hiyo nakuahidi kuendelea kuzingatia taratibu na kanuni za ufugaji zilizopo ili kuepukana na migogoro hiyo.