Storm FM

Marufuku kubeba watoto kwenye Matanki ya mafuta Geita

14 April 2021, 6:52 pm

Na kalechongela:

Wananchi  Geita wameiomba serikali ya mkoa wa  kupitia  kitengo cha usalama barabarani  kudhibiti suala na ubebaji wa watoto kwenye matanki ya mafuta kwenye pikipiki.

Hayo yameelezwa na baadhi ya wakazi wa Geita  wakati wakizungumza na Storm FM  nakusema kuwa kumekuwepo na changamoto ya ubebaji wa watoto mbele ya pikipiki hali ambayo ni hatari kwa usalama wa maisha ya watoto.

Kwa upande wao baadhi ya madereva pikipiki wamekiri kuwepo  kwa changamoto hiyo  na kubainisha kuwa mojo kati ya sababu ambayo inasababisha hali hiyo ni sababu za kiuchumi.

Mkuu wa kitengo cha usalama barabani Mkoa wa Geita RTO Salehe Rajabu Digega  amepiga marufuku ubebaji wa watoto mbele ya pikipiki nakwamba atawachukuliwa hatua kali za kisheria  baadhi ya madereva pikipiki watakao kiuka maagizo hayo.

Digega RTO Mkoa wa Geita