Sibuka FM

RUWASA yakabiliwa na uhaba wa vitendea kazi, wataalam

19 November 2023, 4:58 pm

Pichani:Baadhi ya wakuu wa Idara wakiwa kwenye Baraza la Madiwani lililoketi Novemba 07,Mwaka huu ,Ukumbi wa Halmashauri ya Maswa Simiyu.Picha na Alex Sayi

(RUWASA) ndani ya miaka miwili ya utawala wa awamu ya sita wa Rais Samia Suluhu imefanikiwa kutoa huduma ya maji vijijini kwa asilimia 74.

Na Alex Sayi

Wakala wa Maji Safi na Mazingira Vijijini wilayani Maswa mkoani Simiyu RUWASA umebainisha kuwa unakabiliwa na ufinyu wa vitendea kazi vya kutosha ikiwemo ufinyu wa bajeti, magari na rasilimali watu.

Hayo yamebainishwa na meneja wa mamlaka hiyo wilaya hapa  Mhandisi  Lukas Madaha wakati akitolea taarifa ya utekelezaji wa wakala huyo mbele ya madiwani kwenye baraza lililoketi Novemba 07 mwaka huu kwenye ukumbi wa halmashauri.

Mhandisi Madaha amesema kuwa hali ya upatikanaji wa maji kwa  miaka miwili sasa  wilayani Maswa  umefikia 74% kutoka 68% za awali, kufuatia serikali ya awamu ya sita kumwaga fedha nyinga kwa (RUWASA).

Pichani:Meneja wa (RUWASA)Maswa Mhandisi Lukas Madaha,Picha na Alex Sayi
Sauti ya Meneja (RUWASA) Maswa Mhandisi Lukas Madaha

Sanjari na hayo baadhi ya madiwani waliendelea kuhoji juu ya utendaji  kazi wa wakala  huyo kwa kushindwa kutoa huduma ya maji kwa baadhi ya kata, Sadick Duttu Diwani wa kata ya Senani alitaka kujua lini kituo cha afya Senani kitapata huduma  hiyo ya maji.

Sauti ya Sadick Duttu Diwani wa Kata ya Senani

Diwani wa kata ya Mwandete Juliana John amesema kuwa wananchi wa kata hiyo kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na adha ya upatikanaji wa maji hasa wakati wa kiangazi hali inayopelekea wananchi wa kata hiyo kununua maji dumu moja kwa shilingi elfu moja na mia moja.

Sauti ya Diwani wa Kata ya Mwandete Juliana John

Diwani wa kata ya Budekwa wilayani hapa Esther Ng’holongo  amesema kuwa hali ya upatikanaji wa maji katani hapo ni mbaya kwa kuwa wananchi wanalazimika kutumia hadi  siku mbili kupata maji yanayopatikana mtoni.

Pichani:Aliyesimama ni Diwani wa Kata ya Budekwa Esther Ng’olongo.Picha na Alex Sayi
Sauti ya Diwani wa Kata ya Budekwa Esther Ng’olongo