Sibuka FM

DC Maswa atekeleza agizo la Makonda, akabidhi ng’ombe 20

16 November 2023, 8:38 pm

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Maswa Onesmo Makota akizungumzia kukabidhi ng’ombe kwa Bi Felister Jayunga baada ya agizo la Katibu Mwenezi CCM Paul Makonda

Na Nicholaus Machunda

Mkuu  wa   wilaya  ya  Maswa  mkoani  Simiyu Mh.  Aswege  Kaminyoge   ametekeleza   agizo  lililotolewa   na   Katibu  wa  NEC  Itikadi,  Uenezi  na  Mafunzo Paul  Makonda  akiwa  katika ziara  yake  wilayani  Busega  la  kumkabidhi   Felister  Jayunga   mama  aliyeibiwa  ng’ombe   wake.

Sauti ya DC Kaminyoge wakati akikabidhi ng’ombe kwa Bi. Felister Jayunga.

Mwenyekiti  wa  CCM wilaya ya Maswa Onesmo  Makota amempongeza Ndugu  Makonda  kwa  jitihadi  hizo  za  kuwasaidia  wananchi wanyonge  hali hali inayoleta  matumaini  kwa chama.

Sauti ya mwenyekiti wa CCM wilaya ya Maswa wakati wa kukabidhi ng’ombe.

Naye mama aliyeibiwa ng’ombe amekishukuru  Chama Cha Mapinduzi kwa kumnunulia mifugo yake   ambapo alikuwa amehangaika kwa muda mrefu  kupata haki  yake.

Sauti ya Bi Felister Jayunga baada ya kukabidhiwa ng’ombe wake waliokuwa wameporwa.
picha ya Bi Felister Jayunga