Sibuka FM

Miradi mitatu iliyochunguzwa na Takukuru  Simiyu  yakutwa   na  dosari

2 June 2023, 7:16 pm

Taasisi  ya  Kuzuia na  Kupambana  na Rushwa  mkoa  wa  Simiyu   imebaini  kuwa  miradi  3  kati  ya  14  yenye  thamani  ya  zaidi ya  bilioni 1 iliyofuatitiliwa   imebainika  kuwa   na  dosari  katika  utekelezaji  wake .

Akitoa  taarifa  katika  kipindi  cha  robo  ya  tatu  ya  mwaka  wa  fedha  2022/2023  Januari  hadi  Marchi, 2023 Naibu  Mkuu  wa  Takukuru  Mkoa  wa  Simiyu   Aron Misanga  amesema  kuwa   miradi  iliyofuatiliwa  inahusisha  sekta  za  afya, elimu  na  barabara.

                   Sauti ya  Aron Misanga

Naibu  Mkuu  wa  Takukuru  amesema  kuwa  jamii  imekuwa   na  ushiriki  mdogo  katika  miradi  ya  maendeleo  hali  inayopelekea  miradi  kujengwa  chini  ya  kiwango  na  kutoleta  tija  na  manufaa  ya  sasa na ya baadaye.

               Sauti ya  Aron Misanga

Katika  hatua  nyigine   Takukuru mkoa wa  Simiyu  imefanya  uchambuzi  wa  mifumo  katika halmashauri ya Maswa,  Meatu ,  Itilima  na   Bariadi  Mji  kwa  lengo  la kutathmini  sheria   na kanuni za utekelezaji  wa  majukumu.

    Sauti ya  Aron Misanga

Aidha  Misangu  amesema  kuwa katika  Programu  ya  Takukuru  Rafiki  wamefanikiwa  kuongeza  wigo  wa  ushiriki  katika  mapambano  dhidi  ya  rushwa  kwa  kuibua  kero  katika  jamii  zao  na  kuziwekea  mikakati ya  kuzitatua.

          Sauti ya  Aron Misanga