Sibuka FM

Halmashauri  Kuu CCM wilaya  Maswa  yaridhishwa utekelezaji ilani  ya  chama

22 May 2023, 12:30 pm

Halmashauri  Kuu  ya  CCM  wilaya  ya  Maswa  imeridhishwa  na  utekelezaji  wa  ilani  ya  CCM  ya   mwaka 2020-2025.

Akitoa  taarifa  kwa  wajumbe  wa  Halmashauri  Kuu ya  CCM,  mkuu  wa  wilaya  ya  Maswa  Mhe,  Aswege  Kaminyoge  amesema  kuwa  katika  kutekeleza  ilani  ya  CCM   kwa kipindi  cha Januari, 2022  hadi  Decemba, 2022  wilaya  ilikuwa  imepokea  zaidi  ya  shilingi  bilioni  30  kwa  ajili  ya  kutekeleza miradi mbalimbali ya  maendeleo.

   Sauti ya DC Maswa Aswege Kaminyoge

Mkuu  wa  wilaya  huyo  amesema  kuwa  katika  utekelezaji  wa  ilani  ya  CCM  ya 2020/2025  katika kipindi  cha  Januari  hadi Disemba 2022  wilaya ya  Maswa  imefanikiwa kuongeza   zahanati, vituo  vya  afya na huduma  zingine  ikilinganishwa  na  kipindi  cha  nyuma.

          Sauti ya DC Maswa Aswege Kaminyoge

Kwa  upande  wa  Kamati  ya  Siasa  ya  wilaya  iliyotembelea   miradi mbalimbali  inayotekelezwa   na  serikali   ya  awamu  ya  sita  chini  ya  Mhe.   Rais  Dkt. Samia  Suluhu Hassan, imetoa mapendekezo na  ushauri    juu  ya  miradi  hiyo  ili  iweze  kuleta  tija kwa  wananchi.

          Sauti ya Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya

Mayunga  George  ni  Mjumbe  wa  Halmashauri  Kuu  ya  CCM  wilaya   amesema  kuwa  ni  vema  viongozi   wa  CCM  ngazi  ya  matawi  na  kata  wakasikiliza  kero  za  wananchi  na  kuziwasilisha serikalini  ili zitafutiwe  ufumbuzi .

        Sauti ya Mayunga George- Mjumbe wa Halmashauri Kuu

Aidha  Halmashauri  Kuu  ya  CCM   wilaya  ya  Maswa  imempongeza  Rais   na  mwenyekiti  wa  CCM   taifa   Mhe.  Dkt  Samia  Suluhu  Hassan  kwa  kazi  nzuri  anayoifanya  katika  taifa  na  wilaya  ya  Maswa  kwa kuleta  fedha  nyingi  kwa   ajili  ya  miradi  ya  maendeleo.

   Sauti ya Mathias Shitagisha Katibu wa CCM -Maswa

Hapa chini ni picha za matukio ya Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Maswa