Sibuka FM

“Changamkieni  Fulsa za  Udhamini wa Mikopo kutoka  PASS TRUST  ili  Mjikwamue Kiuchumi    DC  Bariadi  Simon  Simalenga”

19 April 2023, 5:33 pm

Wananchi  Mkoani  Simiyu wameaswa kuchangamkia  Fulsa  za  Udhamini  wa Mikopo ya  hadi  Asilimia  80%  katika  Miradi  inayochochea  Ukuaji  wa  Uchumi  wa  Kijani katika  Sekta  ya Kilimo, Mifugo  na Mazao  ya  Misitu.

Hayo  yamesemwa  na   Mkuu  wa  Wilaya  ya  Bariadi Mh, Simon  Simalenga   kwa  Niaba  ya  Mkuu  wa  Mkoa  wa  Simiyu  Dkt   Yahaya  Nawanda  Wakati  Ufunguzi  wa  Warsha ya kutoa  Elimu kuhusu  Udhamini wa  Mikopo  na  kampeni  ya  KIJANISHA  MAISHA.

             Sauti ya DC Bariadi Simon Simalenga

Langelika  Kalebi  ni  Meneja  wa Tasisi  ya  PASS TRUST  Kanda  ya  Ziwa  amesema  kuwa  Taasisi  hiyo  imekuwa  ikitoa   Udhamini  wa  Mikopo  kuanzia  Asilimia  20%  hadi  60%  huku  kundi  la  Wanawake  Wanaofanya Miradi   inayogusa  Uchumi  wa  Kijani  ikifikia hadi Asilimia  80%.

            Sauti ya Meneja Pass Trust Kanda ya Ziwa – Langelika Kalebi

Aidha kwa  Upande wake  Afisa  Kilimo  Mkoa  wa  Simiyu  Bi  Kija  Kayenze  amesema  kuwa  Wakulima  wengi  wa  Mkoa  wa  Simiyu  wapo  maeneo  ya  Vijijini  hivyo kuitaka  Taasisi  ya  PASS TRUST   itumie  kila  aina  ya  njia ili  kufikisha  Elimu  hiyo kwa Wakulima  ili  Wajikwamue  Kiuchumi..

            Sauti ya Afisa Kilimo Mkoa wa Simiyu – KIJA  KAYENZE

Kwa Upande  wa  Wakulima,  Wafugaji  na  Wafanya Biashara  Mkoani  hapa  Wameishukuru  PASS TRUST  kwa  kuja na njia hiyo ya  kuwakomboa   kwani  mara  nyingi wamekuwa   wakienda  kukopa Fedha  kwenye Taasisi  za  Kifedha  na  kukosa  kutokana  ya  kushindwa kukidhi vigezo  vya  kukopesheka.