Sibuka FM

Father  Mashenene  atoa  Msaada  wa  Baiskeli za  walemavu   S/Msingi  Malampaka.

15 April 2023, 8:10 pm

Baba  Paroko wa  Parokia  ya  Malampaka Jimbo la Shinyanga Padre Renatus Mashenene  ametoa  msaada  wa  Baiskeli mbili  za  Walemavu  kwa shule ya  Msingi  Malampaka  iliyopo  Wilayani  Maswa  Mkoani  Simiyu  ili  kuunga mkono  Jitihada  za  Serikali ya  awamu  ya  sita ya  kuwajali  watu  wenye Makundi maalumu.

Baba Paroko  Mashenene  amesema  kuwa   watu wenye  ulemavu  wana  haki sawa  na  watu  wengine hivyo  wana  haki  za  kupata  mahitaji  yote  ya  Muhimu  ya  Binadamu  huku  akielezea  kuwa  sisi  Binadamu  wote  ni  ndugu tunapaswa  kupendana  na  kuondoa  Ubinafsi  kati  yetu.

Sauti ya Father  Mashenene..

Amesema  kuwa  wakati   mwingine  Mungu  huruhusu  kila  mmoja  Kuzaliwa  Jinsi  alivyo  ili  tu  Mapendo  yake  yatimie    kwani  kila mmoja  ana thamani   mbele  za  Mungu  iwe Masikini  au  Tajiri, Mwembamba  au  mnene,  mdogo  au  mkubwa.

        Sauti ya Father   Mashenene

Akipokea  Baiskeli  hizo  kutoka  kwa  Father  Mashenene,  Mkuu  wa  Wilaya  ya  Maswa  Mhe,  Aswege  Kaminyoge  amemshukuru  Father Mashenene  kwa  msaada   huo  ambao  unaenda  kutimiza  Azima  ya  Serikali  ya  kuwapatia  Mahitaji  Muhimu  watu  wenye  Ulemavu hivyo  wadau  wengine  Waige Mfano  huo.

      Sauti ya DC  Maswa  Kaminyoge

Aidha  Mkurugenzi  Mtendaji  wa  Halmashauri  ya  Wilaya  ya  Maswa   Saimon Berege  amesema  kuwa  Jambo  ambalo  amefaya  Father  Mashenene  linaleta  Baraka  mbele za  Mwenyezi  Mungu  a  kumsihi  asichoke  kusaidia  kwani  uhitaji  kwa  watu  wenye  Ulemavu ni  mkubwa.

          Sauti ya DED Maswa  Saimon  Berege

Akitoa  Taarifa  kwa  Mkuu  wa  wilaya, Afisa  Elimu, Elimu  maalumu wilaya  hapa Abel  Charahani  Lucas  amesema kuwa  Jumla  ya watoto 182  wenye  Ulemavu  mbalimbali katika  wilaya  ya  Maswa ambao wapo  shuleni  wanaendelea  na  Masomo..

         Sauti ya Abel Charahani Afisa Elimu, Elimu Maalumu Maswa

Josephina  Clementi  ni  Mama  Mzazi  wa  mtoto  mwenye  Ulemavu   amemshukuru  Father  Mashenene  kwa  Msaada  wa  Baiskeli  hiyo  ambayo  itamsaidia mwanae  kwenda  shule  kila  siku

    Sauti ya Josephina  Clementi mama mwenye mtoto Mlemavu.

Hapa chini picha za Matukio ya Hafla ya kukabidhi Msaada wa Baiskeli kwa Wanafunzi wenye Ulemavu shule ya Msingi Malampka.