Sibuka FM

SIMIYU:watu (71) hufariki kila siku kati ya vifo 25,800 kwa mwaka kwa ugonjwa wa kifua kikuu (TB).

24 March 2023, 7:49 pm

Kwenye picha ni Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa akihutubia wananchi walijitokeza katika maadhimisho ya Siku ya kifua kikuu duniani ambapo kitaifa yaliyofanyika katika viwanja vya halmashauri ya mji wa Bariadi mkaoni Simiyu hii leo mnamo tarehe 24.03.2023

Na Alex.F.Sayi.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Mhe.Kasimu Majaliwa Majaliwa amesema kuwa kwa siku wagonjwa (71)hufariki kwa Ugonjwa wa Kifua Kikuu kati ya  vifo (25,800) vilivyogundulika  kwa mjibu wa Takwimu za mwaka 2022.

Hayo ameyasema kwenye Maadhimisho ya siku ya Kifua Kikuu Duniani yaliyoadhimishwa Kitaifa Mjini Bariadi Mkoani Simiyu ,huku kauli mbiu ya Maadhimisho hayo ikiwa ni “Kwa pamoja tunaweza kutokomeza Kifua Kikuu Nchini.”

Mhe.Majaliwa amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa Nchi (30) zenye maambukizi ya Kifua kikuu  ambapo kwa pamoja zinachangia asilimia(87%)ya wagonjwa wote Duniani.

Sauti ya Waziri Mkuu ,Mhe.Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa mkoa wa Simiyu wakati wa maadhimisho ya siku ya kifua kikuu duniani.

Kwa upande wake Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema kuwa ugonjwa wa kifua kikuu ni tishio hapa Nchini kwakuwa watu wanaoathirika na ugonjwa wa kifua kikuu ni watu masikini hivyo kuwataka wananchi kujitokeza kupima ugonjwa huo ili waweze kutibiwa kwakuwa ugonjwa huo unatibika.

Sauti ya Waziri wa Afya nchini Mhe.Ummy Mwalimu

Akitoa salamu za Mkoa wa Simiyu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ,Dkt.Yahya Nawanda amesema kuwa anaishukuru Serikali kwa kutoa zaidi ya Tsh Bill 17  kuboresha huduma za Afya Mkoani hapa

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe.Dkt.Yahya Nawanda