Sibuka FM

WAKAZI ZAIDI YA  120,000 WILAYANI MASWA MKOANI SIMIYU HAWAJACHANJA CHANJO YA COVID -19.

March 14, 2023, 5:20 pm

Kwenye picha kutoka upande wa kulia mwenye ni Bi.Fatuma Ally Mahendeka ,mwakilishi wa TADIO akiwa na mratibu wa chanjo wilaya ya Maswa ,Bw.Abel Machibya wakifatilia majadiliano na wadau wa afya katika kikao cha tathmini ya chanjo ya covid-19.

Na Alex Faida Sayi.

Halimashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu kupitia wataalamu wa Afya na waratibu wa chanjo Wilayani hapo imejipanga kuhakikisha inawafikia  wakazi zaidi ya   (120,000) ambao hawakuweza kuchanja chanjo ya  Covid 19,tangu zoezi hilo lilipoanza kutekelezwa Augost.21.2021,huku ikiwaasa  wakazi wapatao (221,324)  waliochanjwa kujiandaa na chanjo ya Busta. 

Hayo yamesemwa  na Mratibu wa  chanjo Wilayani  hapa Bw,Abel Machibya wakati wa Semina yakutathmini changamoto zilizochangia kushindwa kuwafikia wakazi wote Wilayani hapa, Semina iliyofanyika Ukumbi wa Peace Hotel,ikijumuisha Maafisa Afya,waratibu wa Chanjo wilaya na waandishi wa Habari pamoja na TADIO  kupitia ufadhili wa Internews.

Machibya amesema kuwa miongoni mwa changamoto zilizopelekea kutowafikia wakazi wote wa Maswa ilikuwa ni pamoja na uhaba wa vituo vya kutolea Chanjo ya Covid- 19, ambapo awali vituo vya kutolea huduma hiyo vilikuwa ni vituo (4) tu kati ya vituo(51)vya kutolea huduma ya Afya Wilayani hapa ambapo Halmashauri  ina Hospitali (1),Vituo vya Afya(4),na Zahanati(46).

“Kama Halmashauri tulivuka lengo tulilowekewa na Serikali kwa maana tulifanikisha kuchanja wakazi (221,324)sawa na asilimia (102.03%) ya  lengo lililowekwa na Serikali lakuchanja wakazi  zaidi (216,000) sawa na asilimia (60%) ya jumla  ya wakazi wote Wilayani hapa wapatao (344,000) kwa mujibu wa Sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012.

Akitolea ufafanuzi baadhi ya Changamoto zilizochangia kutofikiwa kwa wakazi hao Afisa Afya Wilaya ya Maswa na Mratibu wa Usafi wa Mazingira Bw,Budodi Walwa Walwa amesema kuwa ukiachilia mbali uhaba wa Vituo,kauli mbiu ya Kitaifa yakuchanja kwa hiari Chanjo ya Covid -19 ilichangia kutofikiwa kwa idadi kubwa ya wananchi.

“Kauli mbiu ya kuchanja kwa hiari pia ilitukwamisha na kulikuwa  na mapokeo hasi ya chanjo husika kwa Wananchi waliokuwa wakitilia mashaka ubora wa Chanjo hizo, lakini pia kulikuwa na tetesi ya  baadhi ya Wanachi wenye Group (0)la damu kudai hawawezi kuchanja kwa kuwa kinga zao zipo imara na isitoshe utoaji wa chanjo ulitolewa kwa kubagua baadhi ya makundi ikiwemo makundi ya vijana walio chini ya miaka (18)”Amesema Bw, Walwa.

Bw Walwa ameongeza  kuwa idadi kubwa ya waliojitokeza kuchanja walikuwa ni wanawake,wagonjwa wenye maambukizi ya (VVU)Wazee na watu waliolazimika kuchanja ikiwemo wafanyabiashara na  baadhi ya watumishi Serikalini huku tukiliacha kundi kubwa la vijana.

Walwa amesema kuwa bado kunaulazima wa wananchi na Vijana kujitokeza kuchacha Chanjo ya Covid 19 hasa  wakati huu ambapo Serikali inajiandaa kuzindua Chanjo ya Busta kwa Wananchi.

“Kwa sasa inakadiriwa kuwa  Maswa inazaidi  ya wakazi Laki tano(500,000)kwa mujibu wa Sensa ya watu na Makazi ya mwaka  (2022) Tarafa(3),Kata(36),Vijiji(120)na Vitongoji(510), ukiangalia  Vijana ambo hawakuchanja kwa wakati ule  zoezi linatekelezwa watakuwa wameshavuka umri wa miaka (18)hivyo wanauhitaji wa kuchanja”.Amesema Walwa

 Kwa upande wake Afisa utawala toka Mtandao wa Radio za Kijamii Nchini (TADIO) Bi,Fatuma Ally Mahendeka, amesema kuwa Tadio  kwa ufadhili wa  Internews wanaendelea na zoezi la kuhamasisha utolewaji wa chanjo kwa wananchi Wilayani Maswa na kufuatilia kwa kufanya tathmini ili kuboresha njia zilizokuwa zikitumika kuwahamasisha wananchi kuchanja chanjo ya Covid -19 na kuboresha taarifa zilizokuwa zinatoka kwa wataalamu wa Afya kwenda kwa wananchi baada yakuchanja,kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

“Tunafuatilia mwanzo njia zilizotumika kutoa chanjo kwa wananchi kutoka kwa maafisa afya kwa kujua Idadi ama(takwimu) za wananchi ambao walichanja na ambao bado hawajachanja ili kuweza kutusaidia kuboresha na kuweza kuwafikia hawa ambao hawajachanja,huku zoezi hilo lakufanyia tathmini linafanyika kwa Wilaya ya Maswa tu Nchi nzima.”Amesema Mahendeka.