Sibuka FM

DC Itilima: Wizara tupeni Mamlaka ya Kusimamia Miradi.

February 17, 2023, 12:01 pm

Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu Mhe. Faidha Salim ameishauri Wizara ya Kilimo Kuzipa Halmashauri Mamlaka za Kusimamia Miradi Ili kuondokana na kusuasua Kwa Miradi inayotekelezwa na Wakandarasi.

Mh Faidha ametoa Ushauri huo akiwa Mgeni Rasmi katika Hafla ya Makabidhiano ya Mradi wa Ghala la Kuhifadhia Nafaka uliogharimu Shilingi Milioni Mia tisa na Tisini(Mil 990 )

“Kuna kipindi Mradi huu ulisimama kabisa kwa ajili ya Kusubiri Mkandarasi Mwelekezi na hamna Hatua ambazo tunaweza kuchukua mpaka tufanye Mawasiliano tena na Wizara husika.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima Bi. Elizabeth Gumbo amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Kwa kufanikisha Itilima kupata Mradi huu wa Ghala utakaosaidia Uhifadhi wa Nafaka Wilayani hapo..

Aidha Bi. Gumbo ameiomba wizara ya Kilimo Kuifikiria tena Wilaya ya Itilima katika Mradi ya Umwagiliaji Ili kuzalisha Mazao muda wote hali itakayofanya Ghala hilo liwe na Tija kwa Wananchi na Halmashauri..

Ghala
Dc Itilima(mwenye Ushungi) akikagua Ghala
Dc Itilima akiongea katika Hafla ya Makabidhiano ya Ghala