Sibuka FM

Bilioni 4.2 Kutengeneza  na  Kukarabati  Barabara wilayani Maswa

1 February 2023, 2:38 pm

Wakala  wa   Barabara  za  Mjini  na  Vijijini ( TARURA)  Wilayani  Maswa  Mkoani  Simiyu  imepanga  kutumia   Zaidi  ya  Tsh, Bilioni 4.22  kwa  mwaka  wa  Fedha 2023/ 2024  katika   Kukarabati na  Kutengeneza  Mtandao  wa  Barabara..

Akiwasilisha  Taarifa  ya  Makadirio  hayo  ya  Fedha kwenye Kikao  cha  Baraza  la  Madiwani, Kaimu   Meneja  Tarura  Wilayani  hapa  Mhandisi  Francis  Kuya  amesema  kuwa  Bajeti  hiyo  imezingatia  Vipao mbele  vilivyoibuliwa  na  Wananchi   na  Hali  ya  Upitikaji.

Sauti ya  Mhandisi  Francis  Kuya

Katika Bajeti Mhandisi Kuya amesema kuwa Fedha hizo zinatokana na Mfuko wa Barabara, Mfuko wa Jimbo na Pamoja na Tozo za Mafuta kama anavyoeleza.

Sauti ya Mhandisi Francis Kuya

Nao Baadhi ya Madiwani (Bundala Isambaja Kata ya Nyalikungu na Aroni Mboje Diwani wa kata ya Binza) wameishukuru TARURA kwa Bajeti hiyo kwani imegusa Mahitaji Muhimu ya Wananchi ambao wanawatumikia,

Sauti ya Budala Isambaja na Aron Mboje

Picha za Matukio ya Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

Kaimu Meneja Tarura -Maswa Eng, Francis Kuya
Baadhi ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa.