Sibuka FM

WANANCHI WA IKUNGU WILAYANI MASWA WAJITOLEA KUJENGA ZAHANATI KUPUNGUZA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI..

August 22, 2022, 2:47 pm

Wananchi  wa  Kijiji  cha  Ikungu  kilichopo  kata  ya  Badi  Wilayani  Maswa  Mkoani  Simiyu  wamejitolea  kujenga   Zahanati   ili  kupunguza  vifo  vitokanavyo  na  Uzazi  na  kusaidia  upatikanaji  wa  Huduma  za  Afya  kijijini  hapo..

Wananchi   hao  wameamua  kuchangishana  michango  kwa  kila   Kaya  ili  kujenga  zahanati  hiyo  kutokana  na  Umbali  mrefu  wanaopata   wa  kufuata  huduma  za  Afya  vijiji  vingine  hali   inayopelekea  kuhatarisha  Maisha  ya  Wakazi  wa  Eneo  hilo

Akizungumza  na  Sibuka  Fm    baada  ya  kutembelewa   Mtendaji  wa  Kijiji  hicho  cha  Ikungu  Ndugu   Ibrahimu  Japheti Lugwasha  amesema  kuwa  wamefikia  hatua  hiyo  baada  ya  Changamoto wanazozipata  za  kufuata  huduma  Umbali  mrefu..

Amesema   kuwa   Akina   mama  wajawazito  wamekuwa  wakipata   shida  hasa   inapofika  wakati  wa  Kujifungua  hali  inayopelekea  Wengine  kujifungulia  njiani  na  wengine   kupoteza  Maisha..

Mbunge  wa  Jimbo  la  Maswa  Magharibi  Mh  Mashimba  Ndaki  amewatembelea  na   Kushiriki  Ujenzi  wa  Zahanati  hiyo  iliyopo  Jimboni  kwake  na   kuwataka  wajenge  mpaka  hatua  ya  Boma  halafu  yeye  atawasaidia   Mbao  na  Bati  na vifaa  vingine  vya  kuezekea  kwa  ajili  ya  kukamilisha..

Mh  Ndaki  amesema  kukamilika  kwa  Zahanati  hiyo  itakuwa  Msaada  mkubwa  kwa  wananchi   wa  Kijiji   cha  Ikungu  na  maeneo  jirani  yanayo  yanayozunguka  kijiji   hicho  kwani   watapata  Huduma  kwa  Ukaribu …

Nao  Baadhi  ya   wananchi   wamemshukuru  Mbunge   wao   kukubali  kuwasaidia  Kuezeka  baada  ya  Nguvu  za  wananchi  kukamilisha  Boma  ili  kuondoa    changamoto  hiyo  iliyokuwa  inapelekea  akina  Mama   Wajawazito  kupoteza  Maisha    wakiwa  njiani  kufuata  huduma  za  Afya..

 

Hapa  chini  ni picha  mbalimbali za  Mbuge  na  wanachi  wa  kijiji  cha  Ikungu  wakishiriki  kusomba  Tofauti  kwa  ajili  ya  kuanzisha  Msingi   wa  Jengo  la  Zahati  kwa  nguvu  za  wananchi..