Sibuka FM

MASHIMBA NDAKI AWAONYA WATENDAJI WANAOTAFUNA FEDHA ZA MICHANGO YA MAENDELEO YA WANANCHI..

July 25, 2022, 6:51 pm

Waziri  wa  Mifugo  na  Uvuvi   na  Mbunge  wa  Jimbo  la  Maswa  Magharibi  Mh  Mashimba  Mashauri  Ndaki  amewaonya  watendaji  wa  vijiji  na  Kata  wanaotafuna  Fedha  za  Michango  ya   Maendeleo  ya  Wananchi wanazowachangisha  kisha  kutowasomea  Mapato  na  Matumizi na   kuwapa  Mrejesho.

Waziri   Ndaki  ameyasema  hayo  katika  Ziara  yake  ya  Kibunge   Katika  Jimbo  lake  la  Maswa   Magharibi  ya  kukagua  na  kuhamasisha  Shughuli  mbalimbali  za  Maendeleo..

Insert   01.  Mashimba  Ndaki

Awali  Mbunge   Ndaki  alisikiliza  Kero  za  Wananchi  wa  Jimbo  lake  kisha  kuzitolea  Ufafanuzi   kupitia  kwa  Wataalamu  alioambatana   nao  katika  Ziara  hiyo..