Sibuka FM

UPATIKANAJI WA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA NA ELIMU YA MASUALA YA AFYA YA UZAZI VYATAJWA KUPUNGUZA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI WILAYANI BUSEGA MKOANI SIMIYU.

27 April 2022, 9:15 am

Imeelezwa  kuwa  Wilaya  ya  Busega  iliyopo  Mkoani  Simiyu  imepunguza  kwa  kiasi  kikubwa  Vifo  vitokanavyo  na  Uzazi  kutokana  na   Upatikanaji  wa  Vituo  vya  kutolea  Huduma   za  Afya  na  Elimu  ambayo  imekuwa  ikitolewa  kupitia  njia  mbalimbali  ikiwemo  Radio  Sibuka  Fm.

Hayo  yamesemwa  na  Mkuu  wa  Wilaya  ya  Busega  Mkoani  Simiyu  Mh, Gabriel   Zacharia   Wakati  akitoa  Taarifa  ya  Utekelezaji wa  shughuli za  Maendeleo  katika  Mwaka  Mmoja  wa  Rais  Samia Suluhu  Hasani  Madarakani  mbele  ya  kamati ya  Ulinzi  na  Usalama  na  Wadau  mbali mbali wa  Maendeleo  wilayani  hapo.

Insert  01. David  Zacharia

Amesema  katika  kipindi  cha  mwaka  mmoja  wa  Rais  Samia  Zaidi  ya  Shilingi Bilioni  mbili  zimeletwa  katika  Wilaya  ya Busega  kwa  Ajili  ya  kutatua  changamoto ya  Huduma  za Afya  ikiwemo  Ujenzi wa  vituo vya  Afya  na  Zahanati, Ukarabati  na  Ukamilishaji  Maboma  yaliyokuwa  yameanzishwa..

Inser  02. David  Zacharia

Mh   Zacharia  amesema  Pamoja  na  kufanya  vizuri  katika  Sekta  ya  Afya   bado  kuna  changamoto  ya  Wilaya kuongoza  kwa  Watoto  wa  kike kukatizwa  ndoto  kwa  kupewa  Ujauzito  na  kuwata  wadau  kushirikiana  kuwafichua  wanaume  ambao  wamekuwa  wakifanya  vitendo  hivyo  vya  kikatii  ili  waweze  kuchukuliwa  hatua  kali  za  kisheria ..

Insert  03.  David  Zacharia.