Sibuka FM

WENYEVITI  WA  VITONGOJI  ZAIDI  YA  40 WILAYANI  MASWA  WAGOMEA  POSHO  YA  ELFU TANO  KATIKA  ZOEZI  LA  UANDIKISHAJI  WA  ANUANI  ZA  MAKAZI  NA  POSTIKODI.

21 March 2022, 8:18 pm

Wenyeviti  wa  vitongoji   zaidi ya   Arobaini  wanaounda  Mamlaka  ya  Mji  mdogo  Maswa  wamegoma   kushiriki  zoezi  la  Uandikishaji  wa  anuani za  Makazi  kutokana  na Kupunjwa   Posho  katika  Zoezi  la  Uandikishaji  wa  Anuani za  Makazi  hivyo kupelekea  kuomba   Mwongozo  wa  Halmashauri  kuhusu  Ulipwaji  wa  Posho  hizo.

Wenyeviti   hao  wakiwa  wamekusanyika  kwenye  Ukumbi  wa  Mamlaka  ya  Mji  mdogo  wamedai  kuwa  zoezi  hilo  ni  gumu  na  linahitaji  Umakini  hivyo  haifai  kulipwa  shilingi  Elfu  Tano  kwa  siku  na  kama  Halmashauri  haina  bajeti   ni  vyema   wakaacha  kushiriki  katika   Zoezi  hilo.

Sauti ya Joseph  Masali- Mwenyekiti  kitongoji –Mwanguhi.

       

Wenyeviti  hao  wamesema  kuwa  mara  nyingi  serikali  imekuwa  ikiwasahau na  kutojali  Masilahi  yao licha ya  wao kuhusika na  zoezi  hilo   moja  kwa  moja   kwani  wao  ndio  wanazitambua  kaya  na  Mipaka  ya  maeneo  yao.

Sauti ya Nkinda  Idama – mwenyekiti wa kitongoji  cha Nyambiti

     

Aidha  wamesema  kuwa  awali  waliambiwa  kuorodhesha  majina  ya  Barabara  kwenye  vitongoji  na Mitaa  yao  na  kuyawasilisha  Halmashauri  kasha  kurudishiwa  Nakala  ili  ziwasaidie  kujua  barabara  zilizopitishwa  na  Halmashauri    huku  wakidai  Zoezi  la  kupata vijana  watakaofanya  kazi za  Kuweka  Anuani  za  Makazi  liligubikwa  na  Urasimu.

Baadhi ya Wenyeviti wa  vitongoji –Mamlaka  ya mji  Maswa

       

Baada  ya  mgomo  huo  na  malalamiko  ya  Kupunjwa  Posho, Mratibu  wa  zoezi   hilo  la  Anuani  za  Mkazi   wilayani  Maswa   Ndugu  Edwini  Bairu   akawasilisha  Mwongozo  wa  Halmashauri ya Maswa   kuhusu  utaratibu  wa  Ulipwaji  wa  Posho za  wenyeviti  wa vitongoji  na  Mitaa  na kuahidi  kuwaongezea  elfu Tano  ili  ifike  Elfu  kumi  ili  wakafanye  Zoezi  hilo   Muhimu.

Sauti ya Edwin   Bairu- Mratibu wa  zoezi  la Anuani  za  makazi

   

Hapa chini ni baadhi ya wenyeviti wa vitongoji wanaunda Mamlaka ya Mji mdogo Maswa.

Mwenyekiti wa Mamlaka ya Mji mdogo Maswa (aliyenyoosha mikono) akiwa na Mratibu wa Uandikishaji wa Anuani za Makazi Maswa Edwini Bairu (aliyevaa shati Nyeupe)
Wajumbe wa Mamlaka ya Mji Mdogo Maswa