Sibuka FM

Wadau  wa  afya  waombwa kujitokeza  kusaidia upatikanaji wa vifaa vya kulelea watoto njiti ili  kupunguza vifo  vya  watoto  wilayani Maswa.

28 February 2022, 3:45 pm

Taasisi na wadau mbalimbali wa afya wameombwa kujitokeza  kusaidia upatikanaji wa vifaa vya kulelea watoto njiti katika hospitali ya wilaya ya Maswa ili kupunguza  vifo  vya  Watoto  na  kuiongezea hospitali hiyo uwezo wa kuwahudumia watoto  wengi wanaohitaji huduma hiyo kwa wakati mmoja.

Mganga Mfawidhi  wa hospitali hiyo Dk. Bwire James Robert amesema kuwa kwa sasa wanao  uwezo wa kuwahudumia watoto 10 kwa  wakati  mmoja, kutokana na msaada wa vifaa uliotolewa na taasisis isiyokuwa ya kiserikali ya Dorice Mollel Foundation.

Aidha Dk  Bwire   amesema  kuwa huku  uhitaji wa vifaa hivyo hospitalini hapo bado ni mkubwa, hivyo kuwaomba wadau mbalimbali wa afya kuendelea kujitokeza na kusaidia upatikanaji wa vifaa hivyo kwa ajili ya watoto njiti.

Sauti ya Dk Bwire Robert

 

Dk   Bwire  amevitaja vifaa ambavyo wamevipata kwa msaada wa Dorice Mollel Foundation na kusema kuwa vimesaidia kwa kiasi kikubwa utolewaji wa huduma kwa  watoto njiti na kwamba tangu vifaa hivyo wiwasili hospitalini hapo  vimesaidia kuepuka  vifo  kwa   watoto  Njiti   na  hawajatoa  rufaa kwa watoto kwenda  kutibiwa Bugando..

Sauti ya Dk Bwire Robert

    

Kwa upande wake Dorice Mollel ambaye ni mkurugenzi wa taasisi ya Dorice Mollel Foundation ameeleza kuwa kilichowasukuma kutoa  msaada wa vifaa hivyo  ni kutokana na changamoto ya matibabu kwa watoto njiti  hali  iliyokuwa  inapelekea  wengi  kupoteza  Maisha   kwa  kukosa  huduma  hiyo.

Sauti ya Dorice Mollel

    

Kwa  mujibu wa mganga mfawidhi wa hospitali  ya wilaya ya Maswa Dk. Bwire James Robert  amesema  kwa  sasa  wanapokea watoto njiti 16 – 23  kwa mwezi, kutoka  wilayani humo na maeneo mengine ya jirani na wilaya hiyo..