Sibuka FM

Serikali   Mkoani  Simiyu  kujenga  Mabweni  ya  wanafunzi wa  kike  ili   Kunusuru Mimba  za  Utototni..

25 February 2022, 5:50 pm

Serikali  Mkoani Simiyu  inatarajia kutumia  zaidi ya shilingi  Bilion  6  kujenga  mabweni kwa ajili ya kuwanusuru na  Mimba za Utotoni  watoto wanaotoka  kwenye  kaya masikini  wanaosoma  Shule  za  Sekondari  Mkoani  hapa.

Akizungumza  na wakazi wa Wilayani  Maswa Mkoani  Simiyu kwenye mkutano wa hadhara  uliofanyika  kwenye  viwanja  vya Madeko Mkuu   wa Mkoa   Mh,  David  Zacharia  Kafulila amesema  kuwa  ujenzi huo wa mabweni utaanza  kutekelezwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023..

Sauti ya RC Simiyu- David Kafulila

      

Giladius Michael  Lwezaura  ni  Mwalimu Mkuu  shule  ya  Sekondari  Nyalikungu  iliyopo  wilayani  hapa  amesema  watoto  wa  kike  wamekuwa  wakikutana  na  changamoto  kubwa kutokana  na  kukosekana  kwa  Mabweni  ya  wanafunzi wa  kike..

Sauti ya Mkuu wa Shule Nyalikungu Sec

Aidha  Mwalimu  Eliud  Kabengo  amesema  kuwa  mara nyingi  wanafunzi  wa  kike  wanaporudi  nyumbani  baada  ya  Masomo  ya  Darasani  wamekuwa  wakifanyishwa  kazi  za  majumbani  hali  inayopelekea  kukosa  Muda  wa  kujisomea..

Sauti ya Mw Eliud Kabengo

  

Naye  Monica  Malale  Gogadi   kutoka  shule  ya  Sekondari  Nyalikungu  ameiomba  serikali  ya  Rais  Samia  Suluhu Hasani kuona    Umuhimu  wa kujenga  mabweni  kwa  watoto  wa  kike  ili  kuondoa  changamoto  zinazowakabili  na  kuongeza  Ufaulu  katika   Masomo  yao.

Sauti ya Monica-Mwanafunzi

   

Nao  baadhi  ya  wananchi  wamepongeza  mpango  huo  wa  Serikali  wa  kujenga  Mabweni  kwa  ajili  ya  watoto  wa  kike kwani itasaidia  tatizo  la  Mimba  za  Utotoni  ambazo  zimekuwa  zikitatiza    ndoto  zao.

Sauti ya Baadhi Wananchi -Maswa