Sibuka FM

Katibu  Tawala  Wilaya  ya   Maswa  awaasa    viongozi  kuwatumikia  Wananchi..

25 February 2022, 12:30 pm

Katibu   Tawala  wilaya  ya  Maswa  Agnes  Alex  amewataka  viongozi  waliopewa   Dhamana  ya  Kuwatumikia  wananchi     wanawatumikia  kikamilifu  ili  kukidhi  matarajio  yao.

Katibu  Tawala    ameyasema  hayo  wakati  wa  Uzindunduzi  wa   Kikao  cha  Uraghbidhi  kilichofanyika  Februari  22, katika  Ukumbi  wa  Halmashauri  ya  Maswa  na   Kusema  kuwa  wananchi  wamekuwa  na  matarajio  makubwa  kutoka  kwa  Viongozi   wao..

Sauti ya Katibu Tawala -Maswa Agness Alex

                

Bi  Agenss  amesema  kuwa   Takwimu  zilizotolewa  na  Shirika  la  Twaweza  zitawasaidia  katika  kushughulikia  Changamoto  zinazowakabiri  wananchi  wa  Wilaya  Maswa  na  siyo  kuzibeza  na  kuzikosoa   kwani  zimetoka  kwa  Wananchi  Wenyewe..

Sauti ya Katibu Tawala -Maswa Agness Alex

                

Awali  akiwasilisha  Taarifa  ya  Shughuli  za  Uraghbishi   wilayani  Maswa,  Afisa  Mwandamizi  kutoka  Shirika  la  Twaweza    Richard  Temu   amesema  kuwa   katika  Tafiti  zao  walibaini  kuwa  wananchi  hawahudhurii   mikutano   ya  vijiji  kwasababu  haizungumzii  vipao mbele  vyao  badala  yake  viongozi  kuja  na  Ajenda  zao  na  siyo  kusikiliza  kero  za  Wananchi.

Sauti ya Richard Temu- Afisa Mwandamizi Twaweza

             

Steven  Dwese  ni  Diwani  wa  Kata  ya  Ng’wigwa  iliyopo  wilayani  Maswa  amesema  kuwa  ni  kweli  wakati  mwingine  wamekuwa   wakiitisha  mikutano  ya  vijiji  lakini   wananchi  hawajitokezi  kwa sababu  ya  mgongano  wa  kisiasa   kwenye  maeneo  yao.

Sauti ya Steven Dwese – Diwani kata ya Ng’wigwa

              

Naye  Meneja  program  kutoka  shirika  la  KASODEFO  Marius  Isavika  amesema  kuwa  baada  ya  shughuli  za  uraghabishi   kumekuwepo  na  Hamasa  kubwa  kwa  viongozi  na   wananchi  kushiriki  mikutano  ya  hadhara  kwa   ajili  ya  kujadili  shughuli  za  maendeleo  yao..

Sauti Marius Isavika – Meneja Program Kasodefo

               Hapa chini ni Picha za Matukio ya Uzinduzi wa Uraghbishi -Maswa , Simiyu