Sibuka FM

KILELE  CHA  WIKI  YA  SHERIA , MAHAKAMA   YA  WILAYA  MASWA  YAPOKEA  MALALAMIKO 345 , UTELEKEZWAJI   WA   WATOTO  WAONGOZA..

8 February 2022, 9:44 am

Mahakama  ya  Wilaya  ya  Maswa  Mkoani  Simiyu  imepokea  jumla  ya  malalamiko  345 katika  wiki  ya  sheria  huku  malalamiko  ya  utelekezwaji  wa  watoto  yakiongoza yakifuatiwa  na  Migogoro ya  Ardhi.

Akitoa  taarifa  kwa  mgeni  rasimi, Hakimu  Mkazi  Mfawidhi  wa  Mahakama  ya  wilaya  ya  Maswa  Christiani  Lugumira  amesema  kuwa  katika utekelezaji  wa  wiki ya  sheria  mahakama ilikuwa na  jukumu  la  kuwaeleza  wananchi   maboresho  ambayo yamefanyika  kwa  Faida  ya  wananchi

          

Sauti ya Hakimu  Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Maswa Christian Lugumira

Katibu  Tawala  wa  Wilaya  ya  Maswa   Agness  Alex   kwa  Niaba  ya  Mkuu  wa  Wilaya  Aswege  Kaminyoge   amesema  kuwa  Wananchi  bado  wanahitaji  kuelimishwa  juu  ya  masuala  ya  kisheria   kwani  wanahitaji Huduma  ya  Mahakama  kwa  Ukaribu  Zaidi.

 Sauti ya  Katibu  Tawala  Wilaya ya  Maswa- Agness  Alex

Naye  mwakilishi  wa  Chama  cha  Wanasheria  Tanganyika – TLS    Janeth  Masige  amesema  kuwa   sehemu  pekee  ambayo  mwananchi  anaweza  kupata  Haki  yake  ni  Mahakama  ambapo  TLS  ni  wadau  hivyo wananchi  wazitumie  Mahakama  katika  utoaji  haki.

          

Sauti ya Janeth Masige- TLS

Marselina  Francis  ni   Afisa  wa  Jeshi  la  Polis  Dawati  la  Jinsia  na  Watoto  wilayani  Maswa  Amesema  kuwa  kumekuwepo  na  kesi  nyingi  za  utelekezwa  wa  watoto  kutokana  na  Baadhi  wa  wazazi  kuzikimbia  Familia  zao  hali inayopelekea  ongezeko  la  Watoto  wa  Mitaani

          

 Sauti ya  Afisa wa  Polisi  Dawati la Jinsia  na  Watoto-  Marselina  Francis

Baadhi   ya  Watoto  walioshiriki   kilele  cha  wiki  ya  Sheria   wilayani  Maswa  wamesema  kuwa  Serikali  itunge   sheria  Kali  na  kuzisimamia  kwa  wazazi  wanaotelekeza  watoto  wao.

Sauti za Baadhi ya Watoto

            

Maadhimisho  haya  ya   wiki  ya  Sheria  kwa  Mwaka  huu   2022  yamebeba  Kauli  mbiu  ya  DHAMA  ZA  MAPINDUZI  YA  NNE  YA  VIWANDA,  SAFARI  YA  MABORESHO KUELEKEA  MAHAKAMA  MTANDAO.