Sibuka FM

kata saba wilayani bariadi kuunganishwa na miundombinu ya barabara

30 January 2022, 2:59 pm

Kwenye picha ni madiwani wakiendelea na baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Bariadi juu ya rasimu ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2022/2023 katika ukumbi wa shule ya Sekondari Dutwa

Na mwandishi wetu Daniel Manyanga,Simiyu

Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi wameshauri  kuunganishwa kwa kata saba kwa njia ya barabara ili kuwapunguzia adha wananchi kutumia muda mrefu kufika makao makuu halmashauri hiyo yaliyopo Dutwa.
Wameyasema hayo wakati wakipokea taarifa kwenye kikao cha  baraza la madiwani wa halmashauri hiyo cha kupitia rasimu ya bajeti ya matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha 2022/23 kilichofanyika kwenye ukumbi wa shule ya sekondari Dutwa.

Sauti ya mmoja wa madiwa kutoka kata ya Gambosi,Ndg Bahame Kaliwa akichangia hoja ya kuunganisha barabara kwenye kata saba.

Awali akitoa taarifa kaimu meneja wa wakala wa barabara za vijijini na mijini (TARURA  wilaya ya Bariadi  mhandisi Nyamagalula Ndango amesema wanajumla ya km 607.49 huku akiongeza kuwa  halmashauri hiyo   iliidhinishiwa kiasi cha shilingi  bilioni 2.4 kwaajili ya matengenezo ya barabara,makaravati katika utekelezaji wa bajeti kwa kipindi cha Julai 2021 hadi Juni 2022.
Amesema TARURA Bariadi inatekeleza miradi saba yenye thamani ya shilingi bilioni 2.2  kwa mwaka wa fedha 2021/22 na hadi sasa utekelezaji umefikia asilimia 40 huku bajeti ya matengenezo ya barabara ,madaraja na makaravati kwa mwaka wa fedha 2022/23 ukikadiriwa kutumia shilingi bilioni 2.4

kaimu meneja  TARURA wilaya ya Bariadi  mhandisi Nyamagalula Ndango
Mkuu wa wilaya ya Bariadi Lupakisyo Kapange amewaomba madiwani kuwa sehemu ya usimamizi wa barabara huku katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Bariadi Masanja Sallu akishauri wakandarasi kutopewa kazi nyingi

Mkuu wa wilaya ya Bariadi Lupakisyo Kapange