Sibuka FM

IDADI YA  WAJAWAZITO  WANAOJIFUNGULIA   KWENYE VITUO  VYA  AFYA  YAFIKIA   ASILIMIA  96%  WILAYANI  MASWA.

26 January 2022, 7:56 pm

Idadi  ya  akina  mama   wanaojifungulia  kwenye vituo vya  kutolea  huduma  za  Afya   wilayani  Maswa  Mkoani Simiyu  imeongezeka  kutoka  Asilimia 55  kwa  Mwezi  Januar -June, 2021  hadi  kufikia  Asilimia 96.4%   kwa  Mwezi  Julai –Decemba,  2021  huku hamna  kifo  kitokanacho  na  Uzazi  ikilinganishwa  na mwezi  Januari-June, 2021 kukiwa  na  vifo 5  vitokanavyo  na  uzazi…

Hayo  yamesemwa  na   Mratibu  wa  Huduma  ya  Afya  ya  Baba Mama  na  Mtoto wilayani  Maswa Dr  Angella  Ngaiza   wakati   akitoa  Elimu  kupitia  Radio  Sibuka fm  juu  Umuhimu  wa  akina  Mama  kujifungulia  kwenye  vituo  vya  Afya  kwani  inasaidia  kupunguza  vifo  vitokanavyo   na  Uzazi..

Sauti ya Dr Angella Ngaiza-Mratibu wa Huduma ya Afya ya Baba, Mama na Mtoto

       

Dr  Ngaiza  amesema  kuwa  pamoja  na  ongezeko  hilo  wapo  akina  mama  wajawazito  wachache  ambao  hawajapata  mwamko   hivyo  kupelekea  baadhi  yao  kujifungulia  njiani  wakati  wanaenda   kwenye  vituo  vya  Afya  jambo  linalohatarisha  Maisha  ya  mama  Mjamzito.

Aidha  amesema  mafanikio  hayo  yamekuja  kwa  ushirikiano  wa  watoa  huduma  za  Afya,  Wadau mbalimbali  wa  Afya   na  Jamii  kwa  ujumla  hivyo  waendelee  kuwahamasisha  akina  mama  wajawazito  kwenda  kujifungulia  kwenye  vituo  vya  kutolea  huduma   kwani   ni   salama  zaidi  ukilinganisha  za  kujifungulia  nyumbani..

Sauti ya Dr Angella Ngaiza-Mratibu wa Huduma ya Afya ya Baba, Mama na Mtoto

          

Picha za Mratibu wa Huduma ya Afya ya Baba, Mama na Mtoto wilayani Maswa akiwa studio za Sibuka fm akitoa Elimu ya Afya ya Uzazi.