Sibuka FM

WILAYA YA MASWA YATAJWA KUONGOZA KWA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI KWA MKOA WA SIMIYU..

December 29, 2021, 11:50 am

Imeelezwa  kuwa  wilaya  ya  maswa  inaongoza  kwa  maambukizi  ya Virusi  ya  Ukimwi (VVU)   Ikifuatiwa  na  Wilaya  Busega  katika  mkoa   wa  Simiyu.

Hayo  yameelezwa  na  Mratibbu  wa  Ukimwi  mkoa  wa  Simiyu   Dr  Hamis   Kulemba  wakati   akizungumza  na  Radio   Sibuka.

Sauti ya Hamis Kulemba -RACC Simiyu

          

Dr  Kulemba  amesema  kuwa  vichocheo  vikubwa  vinavyopelekea maambukizi  kuongezeka  ni  tabia ya  kuwa Wenza  wengi, Wadada  kujihusisha  na  Biashara  za  Ngono  na  pamoja  na  migodi  ya  madini, kambi za  ujenzi  wa  Reli  ya  kisasa (SGR)..

Sauti ya Hamis Kulemba -RACC Simiyu

         

Aidha  Dr   Kulemba  ametoa  wito  kwa  jamii  ya mkoa  wa  simiyu  kila  mmoja  kutambua  VVU  na  Ukimwi  Upo  na  unaua  hivyo  ni  vyema  kupima  na  kutambua  hali  ya  Afya  zetu..

Sauti ya Hamis Kulemba -RACC Simiyu

         

Amesema  kuwa   kuanza  kiliniki  mapema  kwa  mama  wajawazito  kutasaidia kupunguza  watoto  kuzaliwa  na  maambukizi  ya  Virusi  vya  Ukimwi  hivyo kupeekea  kupunguza  vifo  kwa  watoto wanaozaliwa  na  VVU…

……..Mwisho……

Dr Hamis Kulemba RACC Simiyu akiwa Studio Sibuka fm Maswa- Simiyu