Sibuka FM

mtu mmoja afariki na wanne kujeruhiwa baada magari mawili kugongana uso kwa uso

December 24, 2021, 6:52 pm

Kwenye picha ni magari mawili yaliyogongana na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wanne kujeruhiwa wilayani Meatu

Na mwandishi wetu Daniel Manyanga,Simiyu

Mtu mmoja afariki na wengine wanne kujeruhiwa kufuaatia gari lenye namba za usajili T435 AAZ Scania mali ya kampuni ya Turu best na gari lenye namba za usajili T 153 DVX tata mali ya kampuni ya Bashingo trans kugongana uso kwa uso katika Kijiji cha Inonelwa wilaya ya Meatu mkoani Simiyu.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu ACP Blasius Chatanda amesema kuwa ajali hiyo imetokea mnamo tarehe 22/12/2021 majira ya 7:40 asubuhi ambapo amewataja madereva waliosababisha ajali hiyo kuwa ni Ibrahim Ramadhan D/L 4001555161ambaye alikuwa akiendesha gari lenye namba za usajili T 435 AAZ  Turu best Scania akitokea Bariadi kwenda Singida kupitia njia ya Meatu na Evarist Stanslaus D/L 4000872584 ambaye alikuwa akiendesha gari T 153 DVX,Bashingo trans akitokea Meatu kwenda Bariadi na baada ya ajali hiyo wote walikimbia.

Chatanda amemtaja marehemu kuwa ni Elia Safari kondakta wa gari T 153 DVX ambapo mwili wake umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya ya Meatu na majeruhi wengine wanne wakiwa wanapatiwa amatibabu katika kituo cha afya Mwandoya.

Huku chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari T 435 AAZ Turu best kushindwa kuchukua tahadhari kwa watumiaji wengine wa barabara.

“Niwaombe madereva wa vyombo vya moto kuthamini watumiaji wengine wa barabara maana kumekuwepo na tabia baadhi za madereva kujiona wao ndiyo wenye haki ya kutumia barabara hata kushindwa kabisa kuwathamini watumiaji wengine lakini pia jeshi la polisi tutaendelea kusimamia usalama wa watumiaji wote ikiwa pamoja na kusimamia sheria za barabarani kwa ujumla” alisema Chatanda

Hivyo jeshi la polisi mkoa wa Simiyu linatoa wito kwa watumiaji wote wa vyombo vya moto kufuata sheria na kanuni za barabarani.