Sibuka FM

Mkoa wa Simiyu wapunguza vifo vitokanavyo na Uzazi kwa Asilimia 50% Mwezi Julai – Septemba, 2021

27 November 2021, 6:28 pm

Mkoa  wa  Simiyu  umefanikiwa  Kupunguza vifo  vitokanavyo  na  Uzazi  kwa  Asilimia   50%   kwa  Robo  ya  mwezi   Julai,  August  na  mwezi  Septemba 2021  huku   Upatikanaji  wa  Dawa   Ukiongezeka  kutoka  Asilimia  70%  hadi  kufikia  Asilimia  90%.

Hayo  yamesemwa  na   Mkuu wa  mkoa  wa  Simiyu Mheshimiwa David  Zacharia  Kafulila  katika  kikao   kazi  cha  Wadau  wa  Afya  kilichofanyika  Mjini  Bariadi  na  Kusema  kuwa  kupungua  kwa  vifo  hivyo  ni  kutokana  na  Usimamizi  mzuri  wa  Sekta  ya  Afya  kwa  kushirikiana  na  Wadau mbalimbali  wa  Afya

                  

RC KAFULILA
Sauti ya RC Simiyu David Kafulila

Mheshimiwa  Kafulia  amesema  kuwa   mkoa  wa  simiyu  umejipanga  kwa  kila  mtendaji  wa  sekta  ya  Afya  atapimwa  kwa  alama  katika  Utoaji  wa  Huduma  kuanzia  Ngazi  ya  Zahanati  hadi  Mkoa

                  

Sauti ya RC Simiyu David Kafulila

Kwa  upande  wake  Mganga  mkuu  wa  Mkoa  wa  Simiyu  Dr  Boniphace   Malwa  amesema  kuwa  pamoja  na  kufanikiwaa  kupunguza vifo  vitokanavyo  na  Uzazi  kwa   Asiimia  50%    bado  vituo  vingi  vya  afya  havijafikia  Malengo  ya  kutoa  huduma  bora   kwa  Jamii  hali  inayopelekea  malalamiko  mengi  kwa  Wananchi..

                   Insert   03.    Dr  BONIPHACE  MALWA

Sauti ya RMO Simiyu Dr Boniphace Malwa

Aidha  Mratibu  wa  Chanjo  ya  UVIKO -19   Mkoa    wa  Simiyu  akatoa  Taarifa  kuhusu  mwenendo  wa  zoezi  na  Idadi  ya  watu  waliochanjwa  hadi  kufikia mwezi  wa  10, 2021.

Mratibu wa Chanjo ya COVID-19 Simiyu