Sibuka FM

walimu wilaya ya itilima waomba kutatuliwa changamoto zao.

27 October 2021, 2:51 pm

Picha ya pamoja ya walimu kutoka halmashauri ya wilaya ya Itilima wakiendelea kupata mafunzo ya kujengewa uwezo katika utendaji kazi zao

Na mwandishi wetu Daniel Manyanga ,Simiyu

Walimu wilayani Itilima mkoani Simiyu wameiomba serikali kuona umuhimu wa kutatua changamoto zao  ili kuongeza hali ya utedaji kazi.

Wameyasema hayo kwenye semina ya kuwajengea uwezo kwenye  majukumu yao viongozi na wawakilishi wa shule wa kutoka Chama Cha Walimu (CWT) wilaya ya Itilima.

Baadhi ya sauti za walimu walioshiriki mafunzo

Awali akisoma risala mbele ya mkuu wa wilaya hiyo ambaye alikuwa  mgeni rasmi katibu wa chama Cha walimu (CWT) wilaya ya Itilima Njile Lufasinza amezitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili walimu huku mhasibu wa chama hicho  Masuka Ikongo amesema swala la kupandishwa madaraja kwa walimu waliokidhi vigezo lipewe kipaumbele na serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Sauti ya katibu wa chama cha walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Itilima

Akijibu namna ya kutatua  changamoto hizo mkuu wa wilaya ya Itilima Faiza  Salim amesema tayari serikali ameanza jitihada za utatuzi wa baadhi ya changamoto zinazowakabili walimu.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Itilima Mhe,Faiza Salim akizungumza na walimu kwenye mafunzo ya uwezo katika kazi zao

Katika hatua nyingine katibu tawala wa wilaya hiyo Firbert Kanyilizu amewataka walimu wenye tabia ya kukopa bila malengo  kuacha mara moja kwani tabia hiyo siyo nzuri.

Sauti ya katibu tawala wilaya ya Itilima Firbert Kanyilizu