Sibuka FM

mvua iliyo ambatana na upepo mkali imeezua nyumba zaidi 50 wilayani bariadi

25 October 2021, 1:18 pm

Moja kati ya picha ya paa la nyumba likiwa limeezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua katika vitongoji vya Ngulyati na Kadoto wilayani Bariadi mkoani Simiyu

Na mwandishi wetu Daniel Manyanga,Simiyu

Zaidi ya 50 zilizopo kata ya Ngulyati iliyopo wilayani Bariadi mkoani Simiyu  zimeezuliwa na upepo mkali ulioambatana Mvua.

Kutokana na hali hiyo mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Bariadi  Lupakisyo Kapange  alilazimika kufika eneo la tukio na kujionea hali halisi  huku akiwaomba wahanga wa tukio hilo kutotumia nyumba zilizoezuliwa badala yake  wajihifadhi kwa majirani  au kwenye shule za msingi na sekondari zilizopo maeneo hayo wakati ambapo serikali inafanya utaratibu wa kuona namna ya kuwasaidia wananchi ambao nyumba zimeezuliwa na upepo huo..

Kapange amesema kuwa katika kitongoji cha Kadoto nyumba 22 zimeezuliwa na kitongoji cha Ngulyati nyumba 30 huku kukiwa hakuna maafa yoyote kwa binadam yaliyotokea.

Sauti ya mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Bariadi ,Lupakisyo Kapange akizungumza na wahanga wa tukio hilo

Nao baadhi ya wananchi waliokumbwa na changamoto hiyo wamesema baadhi ya mabati yamejikunja mengine yamepeperushwa na upepo  huku nyumba nyingine ziking’oka paa lote.

Sauti ya baadhi ya wahanga wa tukio hilo katika vitongoji vya Kadoto na Ngulyati wilayani bariadi