Sibuka FM

Wivu wa mapenzi wapelekea kumuua mke wake kwa kumkata mapanga.

October 19, 2021, 3:25 pm

Kwenye picha ni kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Simiyu ACP Blasius Chatanda

Mwanamke mmoja aitwae  Pili Masonga mwenye  umri wa miaka 28,msukuma mkazi wa Kijiji cha Kulimi wilayani Maswa mkoani Simiyu ameuwawa na mme wake kwa kukatwa mapanga sehemu mbali mbali za mwili wake.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Simiyu ACP Blasius Chatanda amesema tukio hilo limetokea katika Kijiji cha hinduki, kata ya malampaka tarafa ya Sengerema wilayani Maswa mkoani Simiyu mnamo tarehe 18/10/2021, majira ya saa 1:00 asubuhi.

Kamanda Chatanda amesema mwanamke huyo aliuwawa kwa kuchinjwa na panga maeneo ya shingoni upande wa kulia, kichwani upande wa kulia, paja la upande wa kushoto na kiganja cha mkono wa kushoto na aliyekuwa mume wake Golani Ng’humbu mwenye miaka 35 ,Msukuma,mkulima na mkazi wa Kulimi.

Kutokana na kelele alizokuwa anapiga mhanga kuomba msaada wananchi walijitokeza kumsaidia na kufanikiwa kumkamata mume wa marehemu  akiwa ameshika panga, wananchi walifanya mawasilaiano na polisi na ndipo polisi walienda eneo la tukio.

Aidha amesema chanzo cha tukio ni wivu wa mapenzi ambapo mke(marehemu) wa mtuhumiwa  alikuwa anaondoka na kwenda kuishi kwa dada yake Ushirombo wilayani Bukombe mkoani Geita akiwa ameongozana na shemeji yake John Sole Jaba na Watoto wa shemeji yake huyo.

Sauti ya RPC mkoa wa Simiyu ACP Blasius Chatanda akizungumza na waandishi wa habari juu ya tukio la mauwaji.

Hata hivyo Jeshi la polisi mkoa wa Simiyu linatoa wito kwa wananchi kuacha mara moja vitendo vya kujichukulia sheria mkononi.

Sauti ya RPC mkoa wa Simiyu ACP Blasius Chatanda akiwaomba wananchi kuacha mara moja kujichukulia sheria mkononi